ASKARI wa Jeshi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ) Kikosi cha Ikola, Wilaya ya Mpanda, mkoabi Katavi, Mt 100465 PTE Mohamed Shauri (23), amefariki dunia na wengine 11 kujeruhiwa vibaya baada ya gari walilokuwa wakisafiria kupinduka wilayani hapa.
Kaimu Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa Katavi, Joseph Shilinde, alisema kuwa ajali hiyo ilitokea juzi majira ya saa tisa alasiri katika eneo la Mgoroka, barabara ya Mpanda kuelekea Tarafa ya Karema mwambao wa ziwa Tanganyika.
Ajali hiyo ililihusisha gari lenye namba za usajili 2270JW 97, aina ya Land Rover mali ya JWTZ lililokuwa likiendeshwa na MT 100505 PTE Mussa Nahemba likitoka Mpanda kuelekea Ikola, Tarafa ya Karema ambako ipo kambi ya jeshi hilo.
Mwili wa marehemu umesafirishwa kwa ndege ya jeshi jana na kupelekwa kwao Zanzibar kwa mazishi.
CHANZO-TANZANIA DAIMA.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni