Habari

Ijumaa, 13 Desemba 2013

'' IJUE HISTORIA FUPI YA CUF''

 ‘’ Sisi tuliokutana Dar-es-Salam tarehe 20 mpaka tarehe 21 November tumeamua kuunda Chama cha Siasa katika Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania kitakachoitwa THE CIVIC UNITED FRONT CUF chama cha wananchi’’katiba ya Chama cha wananchi CUF. 



Mnamo mwaka 1992 tarehe 20-21 november wakati ndio kwanza chama cha wananchi CUF kinazaliwa kilimchaguwa Bwana Salum Bimani kuwa Mwenyekiti wa muda katika mkutano mkuu wa chama hicho uliofanyika kwenye hotel ya Star light iliopo jijini Daresalam.
 Kuchaguliwa kwa Bwana Bimani kuwa mwenyekiti wa mwanzo wa Taifa wa muda kwa ajili ya kuendesha mkutano mkuu huo ambao ulikuwa na lengo la kuchaguwa viongozi mbali mbali wa chama hicho ulikuja baada ya kuwepo kwa wagombea wengine wawili ambao walishindana na bwana bimani katika kinyanganyiro hicho cha wenyekiti wa muda. Wagombea hao wengine ni Kapten Abbas Barongo alietokea mkoa wa Daresalam pamoja na Mzee Hassan Omar alietokea mkoa wa Tanga,wote wawli hawa walishindwa kwa idadi kubwa ya kura na Bwana Bimani akawa ndio Mwenyekiti wa kwanza wa muda wa chama hichi kwa ajili ya kuendesha mkutano mkuu wa kwanza wa Taifa mnamo mwaka 1992. kwa kupewa nafasi ya Mwenyekiti wa muda. Baada ya hapo kulianza harakati za kuipitisha na kuithibitisha katiba ya chama cha wananchi CUF ya mwaka 1992 ndio baada ya kupitishwa kwa katiba hio uchaguzi ukaanza rasmi wa kuisimamia katiba na kuendesha chama ,ili chama kiweze kwenda ni lazima kuwe na viongozi waliochaguliwa kikatiba. Majira ya jioni siku ya tarehe 21 november ndani ya ukumbi wa Hoteli ya Star light kulirindima chereko na nderemo mara baada ya muda kufika ambapo mwenyekiti wa mkutano huo alitoa matokeo ya kura yaliopigwa . Wajumbe wengi wa chama walikuwa na shauku ya kutaka kujua nani ameibuka kidedea katika uchaguzi huo ambao ulikuwa wa nafasi mbali mbali,huku wengine wakiwa na hofu kubwa kutokana na wasiwasi kama ilivo kwa binadamu. Ndipo Mwenyekiti alipoatangaza matokeo hayo kwa kumtangaza Mh,Jams Kabalo Mapalala kuwa Mwenyekiti wa chama cha wa wananchi CUF Taifa na ndie aliekuwa mwenyekiti wa mwanzo wa chama hicho. Pia alimtangaza Mh,Seif Sharif Hamad kuwa Makamo mwenyekiti CUF Taifa,Shabani Khamis Mloo kuwa Katibu mkuu,Nassor Seif Amour kuwa Naibu katibu mkuu,Hamad Rashid kuwa mkurugenzi wa fedha,Mussa Hajji kombo mkurugenzi wa oganizesheni,Ali Hajji Pandu mkurugenzi wa mambo ya nje,Bi Fatma Magimbi mkurugenzi wa wananwake,na Hamad Massoud mkurugenzi wa haki za Binadamu,na Muhammed Ali Muhammed kuwa mkurugenzi wa Vijana Taifa,Soud Yussuf Mgeni kuwa mkurugenzi wa uchaguzi. Mara tu baada ya kutangazwa rasmi uongozi nzima wa chama harakati za kukitangaza chama zikaendelea kila sehemu Tanzania nzima ingawa kulikuwa na chanagamoto kadhaa nilielezwa na baadhi ya wahusika. Mnamo mwaka 1995 Chama cha wananchi CUF wakati kikiwa na umri wa miaka miwili miwili na mienzi miwili kilishiriki kwa mara ya kwanza katika uchaguzi mkuu wa Zanzibar kuchuana na chama chama tawala CCM,CUF iliweza kushinda viti 24 kati ya hamsini na mkufuatia matokeo ya utata yaliochukua siku nne bila ya kutangazwa mshindi ramsi wa kiti cha uraisi na mwisho wake tume ya uchaguzi Zanzibar kupitia mwenyekiti wake kipindi hicho Bwana Zubeir Juma Mzee aliweza kutangaza matokeo yaliokataliwa na chama cha cha CUF pamoja na Mataifa kadhaa yalioshuhudia uchaguzi huo. Mwenyekiti huyo alimtangaza DK,Salmin A mour kuwa mshindi wa Urais kwa asilimia 50.2 na mgombea wa CUF amabe alikuwa Maalim Seif alipewa asilimia 49.1 haya ndio matokeoa yalioleta utata mkubwa visiwani Zanzibar.

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni