Habari

Jumapili, 20 Oktoba 2013

Madiwani wa CCM na Chadema nusura ngumi zifumuke

NA JOHN NGUNGE

Tukio hilo la aina yake lilitokea majira ya saa 11 jioni katika ukumbi namba 40 uliopo kwenye jengo la Mkuu wa Wilaya ya Arusha.
Mapema Nanyaro aliwasilisha hoja kuhusu ukusanyaji wa ushuru katika Soko la Kilombero, akidai kuwapo kwa ubadhirifu wa ukusanyaji unaosimamiwa na baadhi ya watendaji wa Wilaya ya Arusha akimhusisha pia Mkuu wa Wilaya hiyo, John Mongella.
Lakini kwa upande wake, Diwani wa Kata ya Terati, Julius Ole Sekeyani, alimpinga diwani mwenzake akitaka Mkuu wa Wilaya asishambuliwe kwa kuwa hahusiki na ukusanyaji wa ushuru sokoni hapo na wala hajawahi kufanya hivyo, madai ambayo yalisikika kupingwa na madiwani wengine.
Akitoa ufafanuzi kuhusu hilo, Mweka Hazina wa Jiji, Kessy Mpakata, alisema mkuu wa soko asubuhi anatoa vitabu vya kukusanyia ushuru kwa vijana maalum walioajiriwa kwa kazi hiyo ambao huvirudishwa tena kwake baada ya soko kufungwa majira ya jioni.
Alisema mkuu wa wilaya hahusiki kabisa na utaratibu huo.
Katika hali isiyokuwa ya kawaida iliyodumu kwa dakika chache, wakati maelezo na ufafanuzi huo ukitolewa, Doita na Nanyaro walipandisha jazba na kutaka kumvaa diwani Ole Sekeyani.
Nanyaro alimtaka Ole Sekeyani kuzungumza kwa lugha ya kawaida na siyo ya kejeli na dharau.
Purukushani hizo zilimfanya mwenyekiti wa kikoa hicho, Diwani wa Kata ya Daraja Mbili, Prosper Msofe (Chadema), kuahirisha kikao hicho majira ya saa 12 jioni hadi tarehe nyingine itakayotangazwa.
Mapema Baraza hilo lilitoa muda wa miezi minne kwa watendaji wa Idara ya Ardhi kuhakikisha wanaweka mipaka maeneo ya vyanzo vya maji, milima na barabara kwa lengo la kuzuia ujenzi holela.
CHANZO: NIPASHE JUMAPILI

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni