Na Haroub Hussein
RAIS Mstaafu wa awamu ya sita wa Zanzibar, Mhe. Dk. Amani Abeid Karume, amesema ni vyema kwa viongozi na wananchi wa Zanzibar kutekeleza ipasavyo malengo ya Mapinduzi ya Zanzibar ya mwaka 1964 ,ili nchi iweze kupiga hatua za haraka za maendeleo.
Alisema miongoni mwa malengo ya mapinduzi hayo ni pamoja na kupinga ubaguzi ukiwemi wa dini, ukabila, siasa na aina nyengine za ubaguzi.
Rais Karume aliyasema hayo ofisini kwake Mazizini, wakati wa mahojiano maalum na waandishi wa habari katika kuadhimisha miaka 50 ya Mapinduzi ya Zanzibar.
Alisema Waafrika wa Zanzibar waliamua kufanya mapinduzi baada ya kufanyiwa ubaguzi uliosababisha kukosa haki zao za msingi.
Karume alisema mapinduzi hayo yaliyoongozwa na marehemu Mzee Abeid Karume ndio uhuru kamili wa Wazanzibari baada ya miaka mingi ya ukandamizaji na unyanyasaji.
Aidha alisema baada ya mapinduzi hayo ambayo mwakani yanatimiza miaka 50 ni vyema malengo yake yakaendelezwa na kuwataka viongozi kuacha kushabikia ubaguzi.
Akizungumzia hali halisi wakati Mapinduzi hayo yakitokea, alisema yeye na ndugu yake Ali Karume walikua wamekuja Zanzibar kutoka Nyasa Land (Malawi) baada ya skuli kufungwa.
Alisema mzee Karume alishiriki kikamilifu katika Mapinduzi hayo tofauti na wengine wanavyosema kuwa alikua hayupo Zanzibar wakati mapinduzi yakitokea.
Akizungumzia mafanikio wakati wa uongozi wake, alisema katika mambo ambayo hatayasahau ni pamoja na kuwepo kwa Serikali ya umoja wa kitaifa Zanzibar (GNU) jambo linalompa faraja baada ya miaka mingi ya mifarakano ya Wazanzibari.
Alisema jambo jengine ni kuanzisha Wizara ya Utawala Bora kwa lengo la kuzuia viongozi kutumia madaraka yao vibaya.
Dk.Karume alisema kujenga bandari ya Malindi ni miongoni mwa mambo aliyoyapa kipaumbele kwa kuelewa ni kuendeleza uchumi.
Alisema jambo jengine ni kupeleka umeme wa uhakiki kisiwani Pemba baada ya kukosa umeme wa uhakika kwa miaka mingi.
Alisema katika sekta ya afya aliweza kuanzisha miradi ya kutokomeza malaria iliyokua ikiwasumbua wananchi wa Zanzibar.
Aidha alisema katika uongozi wake mapambano dhidi ya Ukimwi yalipewa kipaumbele jambo lililosaidia kupungua ongozeko la Ukimwi.
Akizungumzia changamoto alizokumbana nazo wakati wa uongozi wake, alisema ni pamoja na kuingia madarakani nchi ikiwa katika hali mbaya kifedha pamoja na kususiwa na nchi wahisani na mashirika ya kimataifa.
Alisema changamoto nyengine ni kutoka chama kikuu cha upinzani (CUF) ambacho kwa wakati huo kilikua kikishutumu sana mambo yanayofanywa na serikali.
Hata hivyo, alisema hakuogopa lawama kwa kuelewa Rais ndiye mwenye dhamana ya mambo yote kwani kulaumiwa ni jambo la kawaida katika utendaji wa majukumu yake.

Hakuna maoni:
Chapisha Maoni