14/09/2013. Timu ya Jamhuri ya Kisiwani Pemba ambayo ni timu kongwe katika ligi kuu ya Zanzibar jana wameelendea kuvurunda katika ligi hiyo kwa msimu huu baada ya kupokea kichapo cha magoli 3-1 kutoka kwa wakongwe wenzao Chipukizi nayo pia ya Pemba.
Iliwachukua
dakika nane tu tokea mchezo huo kuanza kwa Chipukizi kujipatia bao la kwanza
lililofungwa na mshambuliaji wake mpya Ahmed Ali Omar, baada ya kuwa katika
purukushani za hapa na pate katika lango la Jamhuri.
Hata hivyo
licha ya Jamhuri kujitutumua kuweza kulisawazisha goli hilo, lakini hadi timu
hizo zinakwenda mapumziko bado walijikuta wakiwa nyuma kwa goli moja kwa
sifuri.
Alikuwa ni
Ahmed Omar kwa mara nyengine aliyewanyanyua mashabiki wa timu ya Chipukizi kwa
kupachika bao la pili kwa kichwa safi akiunganisha krosi ya Yahya Muhidini.
Mchezaji
aliyetokea benchi akijaza nafasi ya Fakih Mwalimu ndiyo aliyehitimisha kitabu
cha magoli kwa upande wa Chipukizi katika mchezo huo baada ya kufunga goli la
tatu katika dakika ya 65.
Bao pekee na
lakufutia machozi ambalo ndilo goli la kwanza tokea kuanza kwa ligi msimu huu kwa Jamhuri limefungwa na Mohammed Seif katika dakika ya 70.
Ni mchezo
watatu mfululizo huo kwa Jamhuri kuupoteza baada ya mchezo wake wa mwanzo
kunyukwa magoli 2-0 kutoka kwa Kizimbani United, pia akilala kwa magoli kama
hayo kutoka kwa Fufuni S.C.
Mchezo huo
uliingiza jumla ya shilingi laki saba na elfu thelathini na saba, leo itakuwa
ni kati ya Kizimbani na Fufuni katika uwanja wa Gombani.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni