NA MUHIBU SAID
11th October 2013
B-pepe
Chapa
Walisema hayo katika kikao kati ya Kamati za Bunge ya Ardhi, Maliasili na Mazingira na Bajeti na viongozi wa Chama cha Mawakala wa Utalii Tanzania (Tato), kujadili mazingira ya ufanyaji wa biashara nchini katika sekta ya utalii.
Mbunge wa Viti Maalumu (CCM), Dk. Mary Mwanjelwa, alisema serikali inapaswa kuwa macho katika ukusanyaji wa mapato kutoka katika sekta ya utalii.
Mbunge wa Rombo (Chadema), Joseph Selasini, alisema wadau wa utalii kama vile Tato wanatakiwa kuwa mstari wa mbele kushirikiana na serikali katika kuinua sekta hiyo.
“Kwa mfano watalii wanatoka Ulaya kuja nchini kupanda mlima Kilimanjaro. Wanalipa fedha za utalii. Wanafikia Kenya napo wanalipa. Wakifika Tanzania wanalipa tena kiasi kidogo kuliko walizotoa awali,” alisema Selasini.
Akijibu hoja hizo, Waziri wa Maliasili na Utalii, Balozi Khamis Kagasheki, alisema sekta ya utalii nchini inakabiliwa na changamoto kubwa, ikiwamo sheria zilizopitwa na wakati.
Alisema kutokuwapo kwa ushirikiano kati ya Tanapa, Mamlaka ya Ngorongoro, Bodi ya Utalii Tanzania (TTB) na Tato kunachangia kurudisha nyuma maendeleo ya sekta hiyo nchini.
Alisema ufinyu wa bajeti katika wizara husika kuendeleza sekta ya utalii ni kikwazo, na kueleza kuwa sekta hiyo hutengewa Dola za Marekani milioni 3 (Sh. bilioni 5) tofauti na Kenya, ambao hutenga Dola za Marekani milioni 24 (Sh. bilioni 40).
“Kwa mfano mji wa Nairobi peke yake una vitanda 35,000 vya kulala watalii, wakati Tanzania tuna vitanda 32,000. Mombasa wana vitanda 70,000,” alisema Kagasheki.
CHANZO: NIPASHE
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni