Na Ali Issa-Maelezo
Zanzibar
Rais wa Zanzibar na
Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dkt Ali Mohamed Mwenye Suti ya Blue akipata
maelezo kutoka kwa Katibu Mkuu Wizara ya Ardhi,Makaazi Maji na Nishati wakati
alipofanya ziara ya kutembelea Mnara huo wa kumbukumbu ya Mapinduzi ya Zanzibar
ulipo Kisonge mjini Zanzibar. Picha na Makame Mshenga-Maelezo Zanzibar
Rais wa Zanzibar na
Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dkt. Ali Mohamed Shein ameagiza
kufanyika mazungumzo kati ya Mfuko wa Hifadhi ya Jamii Zanzibar ZSSF na
Wizara ya Ardhi,Makaazi Maji na Nishati ili kupatikana Hati miliki katika
eneo la Ujenzi wa Mnara wa Mapinduzi katika eneo la Michezani Mjini
Zanzibar.
Hayo ameyasema leo
alipofanya ziara maalum kuangalia hatua ya ujenzi wa Mnara huo na Kiwanja
cha kufurahishia watoto Kariakoo unaosimamiwa na Mfuko huo.
Amesema kupatiwa hati
miliki ya eneo la Michezani ni suala la kukaa pamoja taasisi hizo husika kwani
eneo hilo linamilikiwa na Serikali na sio la mtu binafsi.
“Nendeni mkazungumze
na watu wa Ardhi mkubaliane halafu nijue mulipofikia haya yote ni maeneo
ya Serikali,”alisema Dkt. Shein.
Alisisitiza
kwamba Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar imeamua kuliendeleza eneo
hilo la Michezani kwa kujenga Mnara utakao kuwa na Maduka na Mikahawa
hivyo kuna haja kukaa na wafanya biashara wa eneo hilo kufanya mazungumzo
na kuwatafutia maeneo mengine ya kuendeleza biashara zao.
“Wafanya biashara
wanapenda maeneo mazuri, sidhani kama watakataa kupatiwa sehemu nyengine ili
kuendeleza biashara zao,”aliongeza Rais wa Zanzibar.
Aidha Dkt. Shein
alifurahishwa na hatua iliofikiwa katika ujenzi wa majengo hayo na kusema
kiwanja cha Kariakoo kinapaswa kuwa cha kisasa na bora kwani kitatoa huduma
nyingi za kibiashara kitakapo malizika.
Hata hivyo alisema
kiwanja cha Kariakoo kimezungukwa na majirani hivyo upo umuhimu
kukaa na majirani hao kwa mazungumzo ili kupatikana usalama wa eneo hilo.
Nae Mkurugenzi
Mtendaji wa Mfuko wa Hifadhi ya Jamii Abdulwakil Haji Hafidh alisema kuwa
kiwanja cha Kariakoo hadi sasa kimeshagharimu shilingi bilioni 10 na mpaka
kitakapomalizika kitagharimu shilingi bilioni 13.5 za Tanzania.
Alisema kiwanja hicho
kinatarajiwa kutoa huduma kuanzia mwakani kwani hatua kubwa ya ujenzi
imekamilika na vifaa vingi vimeshawasili na vinasubiri kufungwa.
Abdulwakili alisema
kuwa kiwanja hicho kitakuwa na huduma zote muhimu kwa binaadamu ikiwemo
maduka, mikahawa na maeneo ya kupambia maharusi na burudani nyengine.
Aliongeza kuwa
ujenzi wa kiwanja hicho utakapo kamilika wataunda bodi maalu
itakayojitegemea kukiendesha.
Wakati huo huo Dkt.
Ali Muhamed Shein alitembelea eneo la Skuli ya Sekondari ya Lumumba na kukemea
tabia ya kuvamia eneo hilo kwa kuchimbwa mchanga na kuligeuza kuwa gereji.
Amesema Serikali
inampango wa kulizungushia uzio na matayarisho yake yamekamilika na
karibuni tenda ya ujenzi itatangazwa ili kuirejeshea skuli hiyo hadhi
yake ya zamani.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni