Na Fatma
Haji Pemba.
Waziri wa Biashara ,Viwanda na Masoko Nassor Ahmed Mazrui ameitaka jamii
zilizo na watu wenye ulemavu kuitikia wito wa serikali ya kuwasajili ili waweze
kutambulika na kujumuishwa katika mipango ya serikali kama ilivyo kwa watu
wengine wenye ulemavu.
Waziri huyo
ameyasema hay oleo alikuwa akiwahubia wananchi mbali mbali waliojumuika katika
maadhimisho ya siku ya watu wenye ulemavu duniani ambayo kitaifa kwa upande wa
Zanibar yameadhimishwa katika uwanja wa Tennis Chake Chake.
Amesema
serikali imekuwa na mipango madhubuti ya kuwasaidia watu wenye ulemavu ikiwemo
kuwapatia elimu,visaidizi na huduma nyengine mbali mbali hivyo sio vyema kwa
jamii kuendelea kuwaficha watoto wao wenye ulemavu.
Hata hivyo
amesema Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar ya Awamu ya Saba imeendelea kudumisha
amani na utulivu katika nchi ili kutoa fursa kwa watu wote wakiwemo watu wenye
ulemavu kuishi katika maisha ya amani.
Mapema
Akisoma risala kwa niaba ya watu wenye ulemavu wa mikoa mitano ya Zanzibar Bi Attie Suleiman Nassor wameiomba
serikali kuzidisha mashirikiano na
jumuiya za watu wenye ulemavu na ulinzi katika kupambana na gharama za kupanda
kwa maisha ili wafaidike muundo wa hifadhi ya jamii iliyopo.
Aidha Bi Attie ameiomba serikali kuwasaidia watu wenye ulemavu kwa kuingiza mahitaji yao katika mipango ya serikali ili kuweza kushiriki kikamilifu katika mipango ya kimaendeleo, sambamba na kutaka mfuko wa watu wenye ulemavu uweze kuwasaidia watu wenye ulemavu katika sekta ya elimu.
Baadhi ya wananchi waliofika katika maadhimisho hayo wamesema bado
kuna changamoto kwa baadhi ya jamii ya kutowapeleka watoto wenye ulemavu katika
vituo vyenye kutoa huduma za watoto wenye ulemavu sambamba na kuwatambua watu wenye ulemavu wa
aina tofauti.
Wamesema kuwa baadhi ya changamoto zinazoendelea kuwakumba watu wenye ulemavu ni kutothaminiwa na baadhi ya madereva wanaoendesha vyombo vya moto hasa gari za abiria wakidai kuwa huondosha magari hata ikiwa mtu mwenye ulemavu ajakaa katika siti au wakati mwengine kuwapitisha katika maeneo ya kushikia.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni