Habari

Jumanne, 9 Desemba 2014

PICHA ZA SIKU YA WATU WENYE ULEMAVU DUNIANI ZILIZOFANYIKA UWANJA WA TENNIS CHAKE CHAKE PEMBA-DISEMBA 3 MWAKA HUU.







Waziri wa Biashara Viwanda na Massoko wa Zanzibar Nassor Ahmed Mazrui akiwahutubia wanachi waliohudhuria  katika Maadhimisho ya siku ya watu wenye ulemavu duniani ambapo kitaifa kwa Zanzibar yaliadhimishwa katika viwanja vya Tennis Chake Chake Pemba Disemba 3 mwaka huu. 

Afisa tawala wa Mkoa wa Kaskazini Pemba akimkaribisha Waziri wa Biashara Viwanda na Masoko kuwahutubia wananchi katika maadhimisho ya siku ya watu wenye ulemavu Duniani.
 Baadhi ya watu wenye ulemavu wakiadhimisha siku ya watu wenye ulemavu duniani huko Chake Chake Pemba.


 Miongoni mwa watu wenye uemavu na wananchi waliohudhuria siku ya watu wenye ulemavu Duniani kisiwani Pemba.

 Mmoja ya watu wsiona kisiwani Pemba akisoma Qur-an ya ufunguzi wa Maadhimisho ya siku ya watu wenye ulemavu Duniani huko Tennis Chake-Chake Pemba.
 Kikundi cha Dufu cha Tumbe kikitoa burudani katika maadhimisho ya siku ya watu wenye ulemavu duniani huko kisiwani Pemba.
 Bi Halima Akisoma utenzi maalum ulioandaliwa katika siku ya watu wenye ulemavu duniani.

 Bi Attie Suleiman Nassor akisoma risala ya watu wenye ulemavu kwa mikoa mitano Zanzibar katika Maadhimisho ya siku ya watu wenye ulemavu duniani.



Baadhi ya watu wenye ulemavu wakibadilishana mawazo na Mwenyekiti wa Baraza la watu wenye ulemavu Zanzibar huko Tennis Chake Chake..

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni