Habari

Jumatano, 10 Desemba 2014

HAMAD RASHID AWATAKA WANANCHI KUWAPUUZA WASIOITAKA KATIBA MPYA.















Na Is-haka Mohamed,Pemba.                                                                                                                    Mbunge wa jimbo la Wawi Hamad Rashid Moh`d amewata wananchi kutumia fursa zilizopo hivi sasa ya kuwa na uhuru wa kwenda popote kutafuta maisha yao ili kujikwamua na umaskini walionao.
Amesema idadi kubwa ya Wanzibar wapatao laki sita na nusu wanaishi na kufanya shughuli za Tanzania bara ni kigezo cha uhuru walionao wananchi wa Zanzibar ya kujitafutia rizki zao za halali na kuondokana na dimbi la umaskini.
Mbunge huyo amesema hay oleo huko katika kijiji cha Mjanaza shehia ya Uwandani jimbo la Wawi mara baada ya kukabidhi mipira ya maji kwa wananchi wa kijiji hicho.
Amezitaja miongoni mwa fursa zitakazopatika Zanzibar kupitia katiba hiyo inayopendekezwa ni pamoja na wananchi wake kuwa na uwanja mpana wa kutafuta maendeleo yao nje ya visiwa hivyo vya karafuu ambavyo amedai kwa sasa haviwezi kuwapatia fursa hizo.
"Kuna Wazanzibar laki sita na nusu hivi sasa huko Tanzania bara na wanafanya shughuli zao za Maendeleo bukheir kabisa,je wote tungekuwa tukibanana hapa si pangewaka moto"alisisitiza Hamad.
Akizungumza juu ya katiba inayopendekezwa Hamad Rashid amewataka wananchi hao kutoshawishika na maneno ya baadhi ya wanasiasa na watu wanaopita kuwashawishi ili waikatae katiba hiyo kwani ni katiba bora kwa wananchi wa Zanzibar.
Hata hivyo amewataka wananchi hao kuachana  na siasa zenye kuendeleza chuki miongoni mwao kwa vile  hazitawaondolea kero zao za  maendeleo zinazowakabili zaidi ya kuendelea kuwadumaza katika dimbi la  umaskini huku wenzao wakiwaacha nyuma kimaendeleo.
Mbunge huyo aliwakabidhi wanakijiji haomipira kuvutia maji yenye urefu wa mita 300 kwa ajili ya kufikisha maji kikijini hapo.
Aidha Hamad Rashid aliweza kukagua tawi la chama cha ADC akiwa ni mlenzi wa Chama hicho kipya cha siasa ambacho viongozi wake wengi walitokea chama cha wananchi CUF.

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni