Sheikh Ibrahim Ismail aliyekuwa anaangaliwa kama mrithi wa marehemu Sheikh Aboud Rogo, ameuawa kwa kupigwa risasi na watu wasiojulikana usiku wa kuamkia leo. Sambamba na sheikh Ibrahim wengine waliouawa ni watu watatu.
Sheikh Ibrahimu na wenzake wanne walikuwa wanaelekea Nyumbani baada ya kumaliza Kuzungumza katika msikiti wa Mussa ulioko mji wa mwambao wa Mombasa, ambapo walivamiwa na watu wasiojulikana na kupigwa
risasi mfululizo maeneo ya karibu nusu kilometa toka kituo cha polisi cha Bamburi.
risasi mfululizo maeneo ya karibu nusu kilometa toka kituo cha polisi cha Bamburi.
Wengine waliokuwa katika gari hilo ni Gadaffi Mohammed ambaye ni Fundi Seremala, Issa Abdallah Shemeji yake Gadaffi ambaye alikuwa dereva wa gari hiyo, Omar AbuRumeisa na Salim Aboud ambaye alinusurika kufa katika tukio hilo.
Akielezea Tukio hilo, Salim Aboud anasema walikuwa wanarudi nyumbani wakitumia gari aina ya Toyota Fun Cargo
wakati walipovamiwa na watu waliokuwa wanatembea kwa miguu na kuanza kuwarushia risasi na gari yao ikakosa muelekeo na kuacha njia.
"Tumewamaliza wote", alisikia wauaji wakisema baada ya kujifanya naye amekufa ambao waliondoka na gari aina ya Mrak X.
Akizungumzia tukio hilo Sheikh Abubakar Shariff maarufu kama makaburi aliyefika eneo la tukio mapema amekihusisha kikosi maalumu cha polisi cha kupambana na ugaidi kwa kusema, "Kikosi cha ATPU kilikuwa hapa, Kwanini wamekimbia?, nini kitafuatia, kwanini wanatuua, sisi hatujawahi kuua mtu yeyote lakini polisi wanawaua waislamu wasio na hatia" alisema na kuongeza.
"Vitendo hivi vinaongozwa na wamarekani na waisraeli, Sheikh ibrahim hakuwa Westgate wakati inavamiwa.
Hawataki kusikia waislamu wanazungumzia Jihadi ambayo ni sehemu ya uislamu kama ni hivyo basi watuue sote".
Asubuhi ya Agosti 27 mwaka jana Sheikh Aboud Rogo
Akiwa katika Gari na familia yake alivamiwa na watu
wasiojulikana na kupigwa risasi 17 na kufariki dunia.
Akiwa katika Gari na familia yake alivamiwa na watu
wasiojulikana na kupigwa risasi 17 na kufariki dunia.
Mauaji ya Sheikh Aboud Rogo yalihusishwa na Polisi wa Kenya na kupelekea vurugu kubwa kwa siku kadhaa baina ya waislamu na Polisi.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni