Viongozi wa ZFA na Wadhamini wa Ligi Kuu ya Zanzibar Grand Malt wa kwanza Manager wa Grand Malt Ndg Emmanuel Mackando, Meneja Masoko wa Grand Malt Ndg. Fimbo Bultallah.Makamu Mwenyekiti wa Barazala Michezo Zanzibar Ndg Khamis Said na Rais wa ZFA Zanzibar Ravia Idarus, wakifuatilia mchezo huo wa funga dimba wa ligi Kuu ya Grand Malt, kati ya Polisi na Jamuhuri imeshinda 1--0.
Mshambuliaji wa timu ya Jamuhuri akimpita beki wa timu ya KMKM katika mchezo wa funga dimba la Ligi Kuu ya Zanzibar Grand Malt, mchezo uliofanyika uwanja wa Amaan, timu ya Jamuhuri imeshinda 1-0, na kuikosesha Ubingwa timu ya Polisi ilitakiwa kushinda mchezo huu ili kutangazwa bingwa, hatimai Timu ya KMKM imeweza kutetea Ubungwa wake kwa kuifunga timu ya Chipukizi kwa mabao 3--2 mchezo uliofanyika uwanja wa Gombani kisiwani Pemba.
Beki wa timu ya Polisi mwenye jezi ya bluu akizua mpira katika mchezo huo wa Ligi Kuu ya Zanzibar Grand Malt.uliofanyika uwanja wa Amaan.Timu ya Jamuhuri imeshinda 1--0
Mshambuliaji wa timu ya Jamuhuri akimpita beki wa timu ya Polisi katika mchezo wa Ligi Kuu ya Zanzibar Grand Malt, ukiwa mchezo wa mwisho wa Ligi hiyo.
Mashabiki wa michezo Zanzibar wakiishangilia timu ya Jamuhuri baada ya kufunga bao laushindi dhidi ya Polisi likiwabao la kwanza katika mchezo huo lilofungwa katika kipindi cha kwanza cha mchezo huo.
Wachezaji wa timu ya Jamuhuri wakishangilia ushindi wao wa bao moja dhidi ya timu ya Polisi kwa kuwafunga bao hilo la kuagia daraja hilo
Chanzo:http://www.zanzinews.com/
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni