Habari

Alhamisi, 3 Oktoba 2013

Mahakama ya ICC yataka mwandishi wa Kenya akamatwe

Mwandishi huyo Walter Barasa anatuhumiwa kuwahonga mashahidi wanaohusiana na mashtaka yanayowakabili Rais wa Kenya Uhuru Kenyatta na  makamu wake William Ruto.
Viongozi hao wanakabiliwa na mashtaka ya kuchochea ghasia zilizofuatia uchaguzi wa mwaka 2007 na 2008.
Mwezi uliopita,makamu wa Rais wa Kenya Ruto alifikishwa mbele ya mahakama ya ICC ya mjini The Hague kuyajibu mashtaka hayo.
Mahakama ya ICC jana ilitoa waranti wa kuwezesha kukamatwa kwa mwandishi habari Walter Barasa kwa tuhuma za kujiingiza katika kesi ya Makamu wa Rais Ruto.
CHAZO- DW KISWAHILI.
Gambia imetangaza kujitoa kwenye jumuiya ya madola baada ya kuwa mwanachama kwa muda wa miaka 48.
Serikali ya nchi hiyo imeeleza kwamba Gambia haitaki tena kuwa mwanachama wa jumuiya ya ukoloni mamboleo.
Mnamo mwezi wa agosti mwaka jana Gambia ilishutumiwa na Shirika la kutetea haki za binadamu kwa kutoa adhabu ya kifo kwa wafungwa tisa kwa kuwapiga risasi.
Zimbabwe ilijitoa kwenye Jumuiya ya Madola mnamo mwaka wa 2003.  

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni