Habari

Jumanne, 1 Oktoba 2013

Polisi 12 wa Msumbiji wahukumiwa kifungo jela



Polisi 12 wa Msumbiji wahukumiwa kifungo jela
Vyombo vya habari nchini Msumbiji vimetangaza kuwa, mahakama moja nchini humo imewahukumu kifungo cha miaka 12 hadi 20 askari polisi 12 kwa kosa la kuyakodisha silaha makundi ya wahalifu.

Duru za habari mjini Maputo zinaeleza kuwa, polisi hao waliyapatia makundi ya wahalifu silaha za aina mbalimbali zikiwemo bunduki aina ya AK-47 mkabala na fedha, silaha zilizotumika katika vitendo vya wizi na mauaji katika maeneo tofauti nchini humo. Silaha hizo zilikodishwa kwa kiasi kati ya dola 75 hadi 100.

Ni vyema kuashiria hapa kuwa, baadhi ya maafisa wa polisi nchini Msumbiji wanapokea mshahara usiozidi kiasi cha dola 200 kwa mwezi, suala linalowafanya wengi wao kushirikiana na magenge ya wahalifu. Zaidi ya hapo ni kwamba, baadhi ya maafisa hao wa polisi hushirikiana kwa njia ya moja kwa moja na wezi wa kutumia silaha na mauaji.

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni