Wanaharakati hao wanadai haki ya kikatiba.Kwa mujibu wa taarifa wanaharakati hao walioshiriki katika mpambano ya kumuangusha madarakani kiongozi wa zamani wa Libya Moammer Ghadhafi mwaka 2011 wanataka kupata haki zaidi katika katiba mpya ya nchi hiyo.
Makabila ya walio wachache nchini Libya ya Waberber,Tubu na Tuareg watapewa nafasi 6 tu kati ya 60 katika tume iliyopewa jukumu la kuandika katiba mpya,ambapo wanataka kujumuishwa katika katiba hiyo lugha,utamaduni na haki yao kama makabila ya Libya.
Watu hao waliteswa chini ya utawala wa Gadhafi na wanahisi kutengwa chini ya utawala mpya licha ya kuwa na dhima kubwa katika vuguvugu la mwaka 2011 lililouondowa madarakani utawala wa Gadhafi.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni