Waasi Mali waombwa kurejea katika mazungumzo ya amani
Mjumbe maalum wa Umoja wa Mataifa nchini Mali Bert Koenders, amewahimiza waasi wa Tuareg na wale wa Kiarabu kurejea katika meza ya mazungumzo pamoja na serikali ya Mali.
Tamko hili lililotolewa hapo jana limekuja baada ya kutokea mapigano mapya Kaskazini mwa nchi hiyo.
Mwishoni mwa mwezi Septemba waasi hao wanaotaka kujitawala katika eneo la kaskazini walitangaza kujitoa katika mazungumzo yoyote ya amani na serikali.
Hatua hiyo ni pigo kubwa kwa juhudi za kutafuta amani katika taifa hilo la Afrika Magharibi lililomchagua rais wake mpya mwezi wa Agosti mwaka huu baada ya kukumbwa na miezi 18 ya msukosuko wa kisiasa uliochangiwa na mapinduzi ya serikali yaliofanywa na wanajeshi walioasi mnamo Machi mwaka uliopita.
Hata hivyo mapigano yalianza tena kaskazini mwa Mali siku moja baada ya waasi kutangaza kujitoa katika mazungumzo ya amani, wanajeshi wawili walijeruhiwa kwa kurushiwa bomu mjini Kidal eneo ambalo ni ngome kuu ya waasi.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni