Bunge la Somalia limepiga kura ya kutokuwa na imani na Waziri Mkuu wa nchi hiyo Abdi Farah Shirdon, baada ya kushindwa kurejesha amani na utulivu nchini humo katika kipindi cha miezi 14 aliyokuwa madarakani.
Spika wa Bunge la Somalia Sheikh Muhammad Othman Jawari amesema kuwa, wabunge 184 walipiga kura za kutokuwa na imani na Waziri Mkuu huku 65 tu wakitangaza kuwa na imani na bwana Shirdon.
Taarifa kutoka Bunge la Somalia zinasema kuwa, hatua hiyo ya wabunge ya kumuondoa madarakani Abdi Farah Shirdon inatokana na kushindwa kwake kufanya juhudi za kurejesha amani na utulivu nchini humo.
Spika wa Bunge la Somalia amesema kuwa, Shirdon ataendelea na shughuli za kiserikali hadi pale Rais Hassan Sheikh Mahmoud atakapomuarifisha Waziri Mkuu mpya ambaye atapewa kipindi cha siku 30 cha kuunda baraza la mawaziri.
Imeelezwa kuwa, hatua ya wabunge ya kupiga kura ya kutokuwa na imani na Waziri Mkuu imetokana na misuguano iliyojitokeza kati yake na rais wa nchi hiyo
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni