Ukosefu utoaji huduma bora, gharama na watendaji wasiokuwa
na ujuzi imesababisha sekta ya utalii
kupungua mapato yake.
Mkurugenzi Mtendaji
taasisi inayotoa huduma za utalii Tanzania ya Travelport Elisaph Mathew
amesema matatizo hayo yamesababisha kupungua idadi ya watalii kutembelea
nchini ikilinganishwa na wanaingia katika nchi wanachama wa jumuiya
ya afrika mashariki.
“Uganda wametembelea watalii laki tisa, Kenya milioni moja
na laki mbili wakati Tanzania
imetembelewa na wageni laki nane wakati imebarikiwa kuwa na vivutio vingi ila
inapata malalamiko tu ju ya utoaji huduma mbaya kwa watalii…” amefahamisha.
Akizungumza katika hafla ya utoaji vyeti kwa wahitimu wa
mafunzo ya utoaji wa huduma za sekta hiyo kwa njia ya elektronic amewataka
wadau wa sekta hiyo kuacha kufundisha watendaji wao kiholela ili kupata
watendaji watakaofanya kazi kwa ufanisi.
nae mkurugenzi mtendaji wa kampuni ya Zenith Tours and
travel Salim Mohamed Suleiman amesema Zanzibar imepata nafasi nzuri katika
kukuza sekta ya utalii na kufikia viwango vya kimataifa katika utoaji wa huduma
kwa watalii.
Mafunzo hayo utoaji wa huduma kwa njia ya elekrtonic ni ya
kwanza Zanzibar yametolewa kupitia kampuni ya Zenith kwa ushirikiano na kampuni
ya Travel port yenye matawi zaidi ya 150
duniani
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni