Habari

Jumamosi, 26 Aprili 2014

Zanzibar yatangaza utalii ASIA

Kamisheni ya utalii Zanzibar inaendelea  kuitangaza Zanzibar kiutalii katika nchi za bara la asia ili kuongeza idadi ya watalii wanaotembelea nchini.

Mwenyekiti wa kamisheni Dr Ahmada Hamadi Khatib amesema wameamua kutafuta zaidi la sekta hiyo ili kuongeza mapato kwani ni sekta tegemo kwa uchumi wa Zanzibar.

Kwa sasa  watalii 13956 kutoka bara la Asia idadi ambayo ni ndogo ukilinganisha na watalii  zaidi ya  laki moja wanotembelea Zanzibar .

?mesema nchi nyingi zinazotegemea utalii hufanya hivyo kutokana na kuwa raia wa bara la Asia wamekuwa na hali nzuri za kiuchumi kutokana na kuwa uchumi mzuri na kutoathirika kiuchumi ukilinganisha na mabara mengine?r Ahmad amezitaja njia wanazotumia ni kueleza mazingira ya Zanzibar, kushiriki maonesho ya kimataifa pamoja na kutayarisha mpango maalum wa kutafuta wakala ili kuondolea usumbufu wa kutoa huduma hizo katika  vituo vingi


Hakuna maoni:

Chapisha Maoni