Godwin Makomba,mmoja ya viongozi walihama Chadema
Waliojivua nyadhifa zao na kujiunga na ACT ni Godwin Makomba, aliyekuwa katibu wa chadema jimbo la Solwa katika halmashauli ya wilaya ya Shinyanga vijijini na mjumbe wa mkutano mkuu wa wilaya,Merikioli Sebastiani, aliyekuwa katibu mwenezi wa kata ya Kambarage, Samweli Dalla aliyekuwa mwenyekiti wa Chadema wa kata ya Kambarage wilaya ya Shinyanga Mjini na Samweli Rafael aliyekuwa mhasibu wa kata ya Kambarage.
Wamesema wameamua kujiunga na ACT kutokana na Chama chao cha awali (Chadema),kutowatendea haki na kutozingatia Demokrasiana viongozi wa ngazi za juu kudharau viongozi wa ngazi za chini na kwamba baadhi ya taarifa za kiofisi zinazowahusu zilikuwa haziwafikii.
“Tumeamua kujivua uanachama kwani viongozi wa ngazi ya juu wamekuwa wakikemea rushwa na kudai demokrasia hasa kwenye uchaguzi wa ndani ya chama uliopita baadhi ya majina ya watu yalichakachuliwa manispaa na kuingizwa majina ambayo hayakutakiwa kwa hilo tutaonekana wanafiki kwa kutoendana na kauli zinazotamkwa”walisema viongozi hao.
Wamesema baadhi ya walioenguliwa bila sababu yoyote kwa mizengwe na kupitia kura za red-brigde ni aliyekuwa mwenyekiti wa wilaya wa chama hicho na diwani viti maalumu Siri Yasin na diwani wa kata ya Kambarage (Chadema) ,aliyekuwa katibu wa mkoa na baraza la wazee taifa Nyangaki Shilungushela.
Mwenyekiti wa ACT, wilaya ya Shinyanga Mjini Suleimani Masoud amethibitisha kuwapokea wanachama hao wapya.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni