Makamu wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar Maalim Seif Sharif Hamad amesema uwekezaji wa hoteli za kisasa zenye hadhi ya Kimataifa, utaisaidia Zanzibar kujitangaza kiutalii, na kuwafanya watalii wa hadhi ya juu pamoja na viongozi wa kimataifa kushawishika kuitembelea Zanzibar.
Akizungumza wakati alipotembela mradi wa ujenzi wa hoteli ya kisasa ya Grand Hyatt huko Shangani amesema kwa kipindi kirefu Zanzibar ina upungufu wa Hoteli zenye hadhi ya kimataifa, hivyo kukamilika kwa ujenzi huo kutasaidia Zanzibar kuwa na hadhi, na kuhamasisha wawekezaji wengine kuwekeza katika sekta mbali mbali za kiuchumi
Nae mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Mji Mkongwe Issa Sarboko Makarani amesema ujenzi huo umezingatia viwango vya Kimataifa na umeridhiwa na Shirika la Umoja wa Mataifa la Elimu, Sayansi na Utamaduni (UNESCO).
Amesema hatua hiyo imefikiwa baada ya mazungumzo ya muda mrefu na shirika hilo linalojishughulisha na urithi wa Kimataifa, ambapo Mji Mkongwe za Zanzibar ni sehemu ya urithi huo.
Makarani amesema hoteli hiyo ya kisasa itakuwa na maegesho chini ya jengo hilo (underground parking), na ni hoteli ya kwanza ya aina yake kujengwa Zanzibar.
Ujenzi wa hoteli hiyo unaotarajiwa kukamilika mwishoni mwa mwaka huu, uta kugharimu dola milioni 35 za kimarekani.

Hakuna maoni:
Chapisha Maoni