Daktari wa meno akimuangalia mtoto wa madrasa matatizo ya meno huko Ziwani Pemba.
Pemba. Jamii
imehimizwa kuwapeleka watoto wao katika madrasa kwa wakati unaofaa badala ya
kuwaachia wakizurura ovyo mitaani bila ya kuwa na chakufanya.
Wito huo
umetolewa na Mjumbe wa kamati ya Madrasat Islamiya ya Ziwani Bw. Hamim Khamis
Kazuba alipokuwa akitoa neno kwenye shughuli maalum ya siku ya afya ya Madrasa
huko Ziwani Chake Chake.
Amesema wapo
baadhi ya watu wanaowachia watoto wao majumbani kwa kipindi kirefu bila ya
kuwapeleka madrasa bila ya kuwa na sababu huku watoto hao wakikosa fursa adhimu
ya kujifunza pamoja na watoto wenzao waliopelekwa katika madrasa.
Mjumbe huyo
amesema kuwa endapo jamii itawajenga watoto wao kwa mafunzo ya elimu mapema
watawajengea msingi bora wa elimu na malezi bora,na kuwahimiza wazee walio na watoto wenye ulemavu kuwapeleka madrasa watoto
hao kwa vile na wao wanayo haki ya
kupata elimu.
Hata hivyo
Mratibu wa Zanzibar Madrasa Resouce Centre Pemba Mwalim Hassan Abdi Bakar
amesema Jumuiya imeendaa siku hiyo maalum kwa ajili ya kuangalia afya za watoto
wa madrasa na watoto wengine ili kujenga afya bora za watoto.
Amesema
kupitia siku hiyo ya afya ya madrasa pia wazazi hupata kuona maonyesho mbali
mbali yanayotokana na mafunzo wanayoyapata katika madrasa hizo.
Mradi huo wa
kutoa huduma za uchunguzi wa afya na lishe kwa watoto wa madraasa hufanywa mara
nne kwa mwaka na jumuiya hiyo katika Wilaya zote nne za kisiwani Pemba.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni