Habari

Jumanne, 18 Novemba 2014

MOMBASA HALI NI TETE, MSAKO WA POLISI MISIKITINI VIJANA WANNE WAFARIKI


 KIJANA alipigwa risasi na kuuawa na wenzake zaidi ya 250 kukamatwa kwenye operesheni kali ya kusaka magaidi mjini Mombasa jana. BAADHI ya vijana waliokamatwa ndani ya misikiti ya Musa na Sakina, eneo la Majengo, Mombasa, wakati wa msako wa polisi usiku wa kuamkia jana ambapo kijana aliuawa na washukiwa zaidi ya 251 kukamatwa.Silaha mbalimbali zikiwemo gruneti, bastola, visu na mapanga zilipatikana ndani ya misikiti hiyo. Picha/LABAN WALLOGA

Akihutubia wanahabari katika kituo cha polisi cha Urban, mjini Mombasa, afisa mkuu wa polisi  (OCPD) Mahmoud Salim, alisema kijana aliyeuawa alijaribu kushamulia maafisa wa usalama kwa gruneti walipokuwa wakiingia msikitini. “Walimpiga risasi kabla ya hajatupa gruneti hiyo na kumwua papo hapo,” akasema Bw Salim na kuapa kuwa operesheni hiyo itaendelea hadi wahalifu wote wanaswe. Vijana 16 walikamatwa ndani ya msikiti wa Masjid Musa na wengine wanane wakapatikana kwenye msikiti wa Sakina. 
Wakati huohuo, viongozi wa eneo la Mombasa wametaka vijana waliotiwa mbaroni waachiliwa mara moja kama hawatapatikana na hatia. 
Wakiongozwa na gavana Hassan Joho, viongozi hao walifika katika makao makuu ya polisi ya kaunti hiyo ambako walishauriana na maafisa wakuu wa polisi kwa karibu saa mbili. 
Walishutumu maafisa wa polisi kwa kuvamia msikiti wakisema ni mahali patakatifu pa ibada. 
Wengine walikuwa Seneta Hassan Omar, Mwakilishi wa Wanawake Mishi Juma Mboko na wabunge Abdulswamad Nassir (Mvita), Rashid Bedzimba (Kisauni) na Badi Twalib (Jomvu). 
- Taifa Leo

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni