Baadhi ya wajumbe na waliokuwa wagombea wa nafasi mbali mbali katika uchaguzi wa ZFA Wilaya ya Chake Chake wakisubiri kupiga kura hapo jana Jumapili.
Na Is-haka
Mohammed,Pemba. Wajumbe
wa Mkutano Mkuu wa Chama cha mpira wa
miguu Zanzibar (ZFA) Wilaya ya Chake Chake kimemchagua Mwalim Amuni Ubwa kuwa
Mwenyekiti mpya wa chama hicho atakayeongoza kwa miaka minne ijayo.
Amuni anayechukua
nafasi ya Ali Bakari Ali ambaye hakugombea nafasi hiyo baada ya kuongoza kwa
mihula miwili alimshinda mpinzani wake Issa Kassim kwa kura 44 aliyepata kura
28 huku kura moja ikiharibika katika kura zote 73.
Nafasi ya
Makamu mwenyekiti ilichuliwa na Khatibu ambaye
alipata kura 62 ambapo nafasi hiyo hakukuwa na mpinzania aliyesimama kugombea
nafasi hiyo.
Aidha
wajumba hao wamemrejesha tena madarakani Suleiman Juma kuwa kuendelea kuwa
katibu wa ZFA Wilaya ya Chake Chake Kwa mara nyengine kwa kumpa kura 59 dhidi
ya 14 alizopata mpinzani wake Hafidh Massoud aliyekuwa katibu msaidizi katika
kipindi kilichopita.
Kwa upande
wa nafasi ya katibu msaidizi aliyechaguliwa ni Ali Amini kwa kura 37 na
kumshinda aliyekuwa mjumbe wa kamati tendaji Nassor Bilal.
Assaa Khamis
Mtwana aliyepata kura 44 na kumshinda Salim Mwadini aliyapata kura 18 alichaguliwa kuwa mjumbe wa
ZFA kamati tendaji anayewakilisha taifa.
Mwenyekiti
wa kamati ya uchaguzi ya wilaya ya Chake Chake Hamad Mzee Shilingi amesema
uchaguzi huo uliendeshwa katika misingi ya uwazi na ulikuwa wa mafanikio ambapo
wajumbe wote na wagombea waliridhika na matokeo.
Akitoa
salamu za wagombea wenzake walioshishiriki uchaguzi huo Salim Haji Mwadini
amewapongeza viongozi waliochaguliwa katika uchaguzi huo na kusema wao
wataendelea kushirikiana na viongozi hao ili kuweza kuendeleza mpira wa miguu
wilayani humo.
MWISHO.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni