KATIKA kijiji cha Mchanga Mdogo, Wilaya ya Wete, Mkoa wa Kaskazini Pemba, jina la Semeni Suleiman Hamad limekuwa mfano wa kuigwa hasa kwa wenye kiu ya kupata maendelkeo kupitia shughuli zao za kila siku kijijini humo Mwanamke huyu mwenye umri wa miaka 39 amebadili mwelekeo wa maisha yake kutoka jitihada za kujikomboa kiuchumi binafsi,na kimazoea na sasa amejikita katika mapambano ya kulinda mazingira dhidi ya athari za mabadiliko ya tabianchi,huku lengo lake kubwa likiwa ni kujikomboa na umasikini wa kipato kukabiliana na mabadiliko ya tabia ya nchi yasiwe kikwazo cha kurudisha nyuma jitihada zake za kujikomboa kiuchumi.
Kupitia juhudi zake, jamii yake wakiwemo akina mama wameanza kumuunga mkono huku wakiwa na matumaini mpya na mshikamano wa kijamii katika kupanda Kandaa, kulinda kuhifadhi na kuitunza ili isiwaletee athari Safari ya Semeni ilianza kupitia mafunzo yaliyobadilisha mwelekeo wake ,yaliotokana na mradi wa Zanzibar Women Leadership Climate Change and Adaptation Zanz Adapt), mradi unaotekelezwa na Jumuiya ya Uhifadhi wa Misitu Pemba (CFP) kwa kushirikiana na Jumuiya ya Uhifadhi wa Misitu Kimataifa (CFI), pamoja na Chama cha Waandishi wa Habari Wanawake Tanzania (TAMWA ZNZ), kwa ufadhili wa Canada Global Affairs.
Mradi huo wa ZANZ ADAPT ambao lengo lake kuu ni kumsaidia mwanamke katika maswala ya kuongeza kipato kwa kukabiliana na mabadiliko ya tabianchi kupitia shughuli zao za kiuchumi ikiwemo kilimo msitu, mboga na matunda, mikoko , pamoja na kuongeza usawa wa kijinsia katika uongozi.Kwa vile yote hayo katika baadhi ya maeneo yamekuwa yanafanyika kimazoea bila utaalamu huku waathirika wakubwa wakiwa ni wanawake , na baadhi ya maeneo yakiwa ni miongoni mwa maeneo yalioathoriwa na mabadiliko ya tabia ya nchi juhudi za kuwasaidia wasiendelee kubaki nyuma kimaendeleo zikawafikia wanawake katika baadhi ya maeneo hayo . Semeni ambae alijengewa uwezo akiwa kama mkulima kiongozi TOT (Trainer of Trainers), na nafasi hiyo ikawa ngazi ya ukombozi kwake na kwa jamii yake akiwa ni miongoni mwa wanawake 4000 ,na wanufaika 16000 waliokusudiwa kufikiwa na mradi huo katika shehia nane Unguja na Pemba.
Awali, Semeni anakiri kuwa haikuwa rahisi kukubali maelekezo ya kitaalamu katika shughuli zake za kilimo,wala kupanda mikoko Lakini baada ya kupata mafunzo, aliamua kuisambaza elimu hiyo kwa wanajamii .
Haikuwa kazi rahisi kukubali mabadiliko ya mtazamo wangu mwanzoni ,nilipokuwa napatiwa mafunzo haya ya kukabiliana na mabadiliko ya tabia ya nchi ,kwa haraka haraka sikuwa naona hasa ayo mabadiliko mpaka nilipoelimishwa nikaelewa ndipo nilipoanza kuziona zile athari zilizopo ndani ya shehia yangu
’’Nilianza kulima kitaalamu kwa kuchanganya jamii ya miti ya mbao na matunda katika shamba moja ,huku sikubweteka nikaanza kupambania mabadiliko ya tabia ya nchi baharini kwa kupanda mikoko na kuwashajihisha wengine ‘’
Ingawa tulichojifunza kupitia mradi nilitakiwa nisaidie kuisambaza elimu hiyo lakini mimi niliangalia baadae nikisema elimu nabaki nayo siitoi jamii yangu itakuja kuwaje nilijisambaz tangia kwa mtu mmoj mmoja hadi sasa sikutaka nibaki nacho peke yangu, bali nimeamua kushirikisha akina mama wenzangu ili tujikomboe na umasikini kwa kupanda mikoko na kulinda mazingira yetu pamoja na kilimo mseto.
Wanawake waliopatiwa elimu sasa wamekuwa walimu wa kupanda mikoko na kuilinda, wakieneza maarifa kwa wengine ambapo kupitia mkulima kiongozi Semeni hadi sasa jumla ya wanawake 91 waliomuunga mkono kupanda mikoko kulinda na kusambaza elimu kwa wengine juu ya kulinda mabadiliko ya tabia ya nchiSidrat Khatib Ali, mmoja wa waliopatiwa mafunzo na Mkulima kiongozi Semeni, yeye anasema,“Urejeshaji wa mikoko umetupa matumaini mapya ya kujikomboa kiuchumi na kulinda bahari yetu yukiamini tunaanda kesho iliyobora ya shehia yetu na vizazi vyetu.
Tulikuwa wahanga wakubwa wa ukataji wa mikoko, lakini sasa tunaona mwanga mpya kwa vile na sisi tumekuwa mawakala wa mabadiliko hayo tunaungana kupanda mikoko na kutoa elimu ya umuhimu wa kulinda
”Kwa upande wake, Khatib Said Khatib, mkulima mwanaume wa Mchanga Mdogo, anakiri,“Nilikuwa napanda mikoko bila utaalamu kwa muda mrefu , lakini sasa nimesimama mstari wa mbele kusaidia wanawake kila wanapokwenda kupanda mikoko,Najua baadae watanufaika wao, lakini pia kutusaidia sisi.
”Maneno haya yanaonyesha jinsi mradi ulivyobadilisha mtazamo wa jamii nzima,si wanawake pekee bali pia wanaume wameungana bega kwa bega katika kulinda mazingira ya baharini .
Mradi wa Zanz Adapt umefika katika baadhi ya shehia ambapo kwa upande wa Pemba ni pamoja ni shehia ya Kambini Kichokochwe,Mjini Kiuyu ,Chwale , pamoja na Mchanga Mdogo ambazo baadhi ya sehemu ya ardhi yake imekuwa miongoni mwa maeneo yasiopungua 3000 zanzibar yalioathika kutokana na mabadiliko ya tabia ya nchi.
Katika maeneo haya, wanawake wameanza kubadilisha maisha yao kwa kupanda mikoko, kujikomboa kiuchumi, na kuwa wawakilishi wazuri wa jamii katika mapambano ya mabadiliko ya tabianchi.
Hadithi za wanawake katika baadhi ya vijiji ndani ya shehia yetu ya mchanga mdogo , yameanza kuzaa matunda nusu na robo wanawake tumebadilika na kuimba mabadiliko ya tabia ya nchi.
Wanawake waliopatiwa elimu sasa wanashiriki kikamilifu katika shughuli za kijamii na hata kuweza kutoa maoni yao linapotokea tatizo au wanapohitaji msaada Wamekuwa sauti ya mabadiliko, wakihamasisha wengine kuacha ukataji wa mikoko na badala yake kushiriki katika urejeshaji wa misitu ya baharini kandaa.
CHANGAMOTO ZINAZOKABILI JITIHADA
‘’Pamoja na mafanikio haya, changamoto bado zipo,Upatikanaji wa mbegu za mikoko ni tatizo kubwa linalokwamisha kasi ya urejeshaji’’.
‘’Aidha, uhitaji wa mafunzo ya kitaalamu zaidi ni muhimu ili kuhakikisha urejeshaji wa mikoko unakuwa wa kudumu na wa kisayansi’’,Yote hayo ni maneno ya semeni Semeni alieleza.
“Tunapanda mikoko, lakini mara nyingine tunakosa mbegu bora. Tunahitaji msaada zaidi wa kitaalamu ili juhudi zetu ziwe na matokeo ya kudumu kwa taifa la baadae.
”Changamoto hizi zinaonyesha kuwa mapambano dhidi ya mabadiliko ya tabianchi yanahitaji mshikamano wa wadau wote, serikali, mashirika ya kiraia, na jamii kwa ujumla.
Juhudi zetu zote hizi hatuoni nguvu ya serikali tunawaza mradi ukimaliza jee nani atakuwa msaidizi wetu wa kutukomboa,na viongozi wetu hawaoni juhudi zetu wanathamini mambo mengine yasio na tija kwetu kama hawapo kabisa USHIRIKIANO NA UONGOZI WA WANAWAKE
Moja ya mafanikio makubwa ya mradi wa Zanz Adapt ni kujenga uwezo wa wanawake kushiriki uongozi Wanawake TOT wamekuwa walimu na viongozi wa jamii, wakitoa elimu kwa wenzao na kuhamasisha mshikamano wa kijamii katika kukabiliana na mabadiliko ya tabia ya nchi.
Kwa mujibu wa Jumuiya ya Uhifadhi wa Misitu Pemba (CFP), katika moja ya maelezo yao kwa waandishi wa habari walisema kuwa asilimia 80 ya wanawake ndio watanufaika na mradi huu waZanz adapt huku asilima 20 ikiwa ni wanaume lengo ni kuwawezesha wanawake kujikomboa na umasikini wa kipato kupitia kilimo mseto ,upandaji wa mikoko pamoja na usawa wa kijinisia .
Jambo ambalo ni hatua kubwa ya katika kuimarisha nafasi ya wanawake katika mapambano ya mabadiliko ya tabianchi hususan ni maeneo ya vijijini .
Mmoja wa viongozi wa CFP alisema Omar Tarika Msellem Akiwa katika Ukumbi wa TAMWA mwanzoni mwa ufunguzi wa mradi huu,Jitihada za Semeni na wenzake zimeleta mabadiliko makubwa ya kijamii na kiuchumi.
Kupanda mikoko si tu kunalinda mazingira, bali pia kunatoa fursa za kiuchumi kupitia kilimo msitu, ufugaji wa samaki, na utalii wa mazingira sambamba na uanzishwji wa vikundi ambavyo vitaunga mkono juhudi hizo.
Wanawake sasa wanajiona kama sehemu ya suluhisho, si wahanga wa matatizo. Wamepata nafasi ya kushiriki katika maamuzi ya kijamii na kisiasa, jambo ambalo awali lilikuwa changamoto kubwa kutokana na mila na desturi,ushahidi wa hilo ni kuziona sauti zao wakisemea kuhusu mabadiliko ya tabia ya nchi kupitia vyombo vya habari ,alisema Amina Ahmed Mohamed kutoka chama cha waandishi wa habari wanawake TAMWA .
Safari ya Semeni Suleiman Hamad ni ushahidi wa nguvu ya elimu na uongozi wa wanawake katika kukabiliana na mabadiliko ya tabianchi. Kupitia juhudi zake, jamii ya Mchanga Mdogo na maeneo mengine ya Pemba sasa yana matumaini mapya ya kulinda mazingira, kujikomboa kiuchumi, na kuendeleza kizazi kinachojali uendelevu wa rasilimali za bahari na ardhi.
Semeni na wanawake wenzake wameonyesha kuwa mapambano dhidi ya mabadiliko ya tabianchi si jukumu la serikali pekee, bali ni wajibu wa kila mwanajamii.
Kwa kupanda mikoko na kulinda kandaa, wameweka msingi wa mustakabali bora wa Pemba na Zanzibar kwa ujumla.Huku Kauli yake ya mwisho inabaki kama dira ya matumaini,“Tunapopanda mikoko, tunapanda pia matumaini ya maisha bora kwa vizazi vijavyo sisi tukishaondoka tumeyaacha mazingira ambayo yanahimili mabadiliko ya tabia ya nchi”MWISHO
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni