Kundi la wanamgambo wenye itikadi kali la Somalia Al Shabab limesisitiza tena hii leo kwamba hakuna mwanamke aliyeshiriki katika hujuma zao dhidi ya jengo la kibiashara jiji Nairobi la Westgate lililosababisha umwagikaji mkubwa wa damu.
Kupitia mtandao wa Twitter kundi hilo limesema sera yao hairuhusu kuwashirikisha wanawake katika operesheni kama hiyo.
Aidha taarifa ya kundi hilo imeendelea kusema kwamba wiki moja baada ya shambulio la Westgate serikali ya Kenya na maafisa wa ujasusi kutoka nchi za Magharibi bado wameshindwa kutambuwa ukweli na kupata maelezo juu ya opereheni hiyo.
Kauli hiyo ya Alshabab yumkini inawekea mkazo kuhusu kushindwa kwa idara za upelelezi kupata taarifa juu ya washambuliaji na maelezo juu ya jinsi tukio hilo lilivyopangwa na kufanyika.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni