24/09/2013
Aidha wanamtaka na Rais Jakaya Kikwete asiusaini Muswada wa Sheria ya Marekebisho ya mabadiliko ya Katiba kwa madai kuwa mchakato huo umehodhiwa na Chama Cha Mapinduzi (CCM).
Kamanda wa Polisi wa Mjini Magharibi, Mkadam Khamis Mkadam, jana alithibitisha kuwa wamepokea barua ya maombi hayo na tayari wameshawaruhusu, lakini kwa kufuata masharti yakiwamo kutotoa lugha za matusi katika majukwaa na kutoa kauli ambazo hazitahamasisha chuki.
Mkurugenzi wa Mawasiliano, Habari na Haki za Binadamu wa CUF, Salum Bimani, alisema tayari maandalizi yameshakamilika na wameshapokea kibali cha kufanya mkutano huo kutoka kwa Jeshi la Polisi ukiwa na lengo la mshikamano wa vyama vya upinzani kuhusu muswaada wa rasimu ya katiba.
Alisema mkutano huo utahusisha chama cha CUF, Chadema na NCCR-Mageuzi. Pia mkutano huo utahudhuriwa na Mwenyekiti wa Kamati ya Maridhiano Zanzibar, Mzee Hassan Nassor Moyo.
Kwamujibu wa Jeshi la Polisi na Bimani, mkutano huo utafanyika katika viwanja vya Kibanda Maiti.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni