Pemba. 18/09/2013
Mufti Mkuu wa Oman
Samahat Shekh Ahmed Bin Hamed Al-Khalil amesema tofauti za madhehemu zilizopo baina
ya waislamu zinaweza kuepukwa ili kuendeleza mashirikiano kwa maslahi ya Uislamu na Waislamu.
Amesema kuendeleza
tofauti na kila dhehebu kujiona bora kuliko mwenzake kunatoa mwanya kwa maadui wa
uislamu kuuhujumu na kuudhoofisha uislamu.
Mufti huyo
Mkuu wa Oman ameyasema hayo leo huko Wete Pemba katika ghafla ya ufunguzi wa msikiti
Mkubwa wa Ijumaa wa Mwitani wenye uwezo wa kuchukua waumini zaidi ya 1500 kwa wakati mmoja.
Amesema
umoja katika uislamu muhimu katika kutekeleza ibada mbali mbali ambalo ndiyo
lengo kuu la kuumbwa mwanadamu
Aidha Shekh
Khalil amewataka waumini wa dini ya kiislamu kuendelea kuisoma Qur-an na kuendelea kuitumia katika kutatua
tofauti zao kwa vile ni chombo pekee kinachoondoa fitna katika uislamu.
Akisoma
risala ya waislamu katika msikiti huo Shekh Abraman bin Hamed bin Haji msikiti huo licha
ya kusaliwa pia kitakuwa ni kituo cha mafunzo ya dini ambapo una jumala ya
madarasa nane ya kusomea ambapo mawili kati ya hayo ni madaraya ya Computa ili
kuwa ni kituo bora cha kutoa elimu ya dini na dunia.
Hata hivyo
amewataka waumini kuutumia vyema msikiti huo pamoja na kushirikiana na kamati
katika kuwekea matunzo pamoja na usafi kwa vile suala hilo ni wajibu wa kila
muislamu.
Mskiti wa
Mwitani uliasisiwa takriban miaka 100 iliyopita na Marehemu Shekh Massoud
Mwitani,ambapo kabla ulikuwa ukifanyiwa ukarabati kila mwaka ili kwendana na
matakwa ya wakati kabla ukarabati huo mkubwa
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni