Polisi katika mji wa Kitale ulioko kaskazini magharibi mwa Kenya wamewakamata watu watatu wanashukiwa kuwa na uhusiano wa karibu na kundi la Al Shabaab la Somalia.
Watu hao wamekamatwa baada ya polisi kupewa taarifa na wakazi wa eneo hilo na kuwakamata watu hao, wakiwemo wanawake wawili raia wa Somalia na mwanaume mmoja kutoka Ethiopia.
Watu hao walikuwa wakijaribu kupanda basi linaloelekea mji wa Lodwar ulioko kaskazini mwa Kenya.
Ofisa upelelezi wa wilaya ya Kitale Linus Owango amesema, watu hao hawakuwa na hati za kusafiria wala vibali vya kisheria vinavyowaruhusu kuingia nchini Kenya.
Amesema watu hao wamefikishwa mahakamani na wataendelea kuhojiwa zaidi na idara ya kupambana na ugaidi.
Wakati huohuo, polisi kwenye wilaya ya Kitale wanawashikilia raia wanne wa Sudan baada ya kuwakamata wakiwa wanaelekea kwenye kambi ya wakimbizi ya Kakuma bila ya kuwa na vibali maalum.
CHAZO RADIO CHINA KISWAHILI.
balozi wa Russia nchini Libya washambuliwa
Wizara ya mambo ya nje ya Russia imesema, ubalozi wa nchi hiyo nchini Libya jana ulishambuliwa na watu wasiojulikana wenye silaha. Watu hao walifaytua risasi na kujaribu kuingia ndani ya ubalozi huo. Hakuna wanadiplomasia wa Russia waliouawa au kujeruhiwa katika tukio hilo.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni