Habari

Jumamosi, 28 Septemba 2013

Mafunzo ya Waandishi Kuripoti katika Mazingira Magumu


Meneja wa Baraza la Habari  Tanzania Suleiman Seif, akifunguwa mafunzo ya Waandishi wa habari kuripoti katika mazingira magumu na kuibuwa vitu ambavyo vinakuwa shida kwa Jamii. mafunzo hayo yameandaliwa na Baraza la Habari Tanzania, na kuwashirikisha Waandishi wa Vyombo mbalimbali vya Binafsi na vya Serekali vilioko Zanzibar.
 Meneja wa MCT Suleiman Seif, akionesha moja ya magazeti  likiripoti habari yamazingira magumu wakati wa ufunguzi huo, uliofanyika katika hoteli ya Mazsons shangani Zanzibar.
 Mtoa Mada kuhusi Uandishi wa habari katika mazingira Magumu Ndimara Tiga akitowa mafunzo hayo kwa waandishi wa habari kuweza kuripoti habari ambazo hazitakuwa na migogoro katika jamii na kuepusha migogoro kutokea, wakati wa mazingira magumu.
 Mtoa Mada ya kuripoti habari za Uchunguzi Joyce akitowa mafunzo hayo kwa waandishi wa habari katika mafunzo ya siku mbili kwa Waandishi wa habari wa Vyombo mbalimbali vilioko Zanzibar.
 Waandishi wakimsikiliza Meneja wa MCT Zanzibar Suleiman Seif, akifunguwa mafunzo kwa Waandishi wa habari Zanzibar kuripoti habari katika mazingira magumu kupata habari, mafunzo hayo yamefanyika katika ukumbi wa hoteli ya Mazsons shangani Zanzibar.
 Waandishi wakijadiliana ninsi ya kuandika habari za mazingira magumu kuepusha migogoro, wakati wa kuripoti habari hizo, kufanya uchunguzi wa kutosha kabla ya kuiripoti katika vyombo husika.

Waandishi wa habari wakiwa katika makundi kujadili namna ya kuripoti habari za mazingira magumu, wakati wa mafunzo yao yalioandaliwa na Baraza la Habari Tanzania MCT, katika ukumbi wa hoteli ya Mazsons shangani Zanzibar.

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni