Waziri wa Afya wa Zanzibar, Juma Duni Haji, amesema hakuna
tatizo kwa kiongozi mwandamizi wa Uamsho, Sheikh Azzan Khalid Hamdan, kutibiwa
nje ya nchi kama jopo la madaktari litapitisha uamuzi huo.
Akizungumza na Mwananchi Ofisini kwake Vuga mjini Zanzibar juzi,
Duni alisema kwa mujibu wa katiba, mwananchi yeyote ana haki ya kutibiwa nje ya
nchi kwa maradhi ambayo tiba yake haipatikani nchini.
Alisema hata hivyo hatua hiyo itategemea uwezo wa Serikali
kifedha na ukubwa wa ugonjwa.
“Bado sijapokea ripoti kuhusu Sheikh Azzan, wajibu wangu
ninapopokea nalazimika kupeleka Hazina, hakuna ombi hata moja nililowahi
kulitupa,”alisema waziri.
Alisema daktari anayemtibu sheikh huyo, anapaswa kuwasilisha
ripoti ya mgonjwa katika Bodi ya Matibabu ya Nje ambayo ndiyo yenye uamuzi wa
mwisho kulingana na ukubwa wa ugonjwa.
Alisema ingawa Sheikh Azzan ni mshtakiwa, hicho hakiwezi kuwa
kigezo cha kukosa kutibiwa nje.
Kiongozi huyo amelazwa katika Hospitali ya Mnazi Mmmoja mjini
Zanzibar akisumbuliwa na maradhi ya figo kuwa na vijiwe na anapaswa kupelekwa
nje ya nchi kwa matibabu.
Katibu wa hospitali hiyo, Omar Abdallah Ali alisema kwa utaratibu
Bodi ya Matibabu ya Nje inakutana kila baada ya miezi miwili kufanya uamuzi
kuhusu wagonjwa wanaotakiwa kutibiwa nje ya nchi.
Alipia pia inaweza kukutana kwa dharura pale panapokuwa na
mgonjwa anayehitaji uharaka wa matibabu.
Kiongozi huyo wa uamsho anakabiliwa na mashtaka ya kufanya
uchochezi na kusababisha uharibifu wa mali za mamilioni y

Hakuna maoni:
Chapisha Maoni