WANAUSHIRIKA wa ‘Nuru njema’ ambao ni
mayatima unaojishughulisha na ufugaji kuku wa mayai, uliopo Mbuguani Wilaya ya Mkoani
Pemba, upo hatarini kutoweka, baada ya kudaiwa kiasi cha shilingi 2,000,000
(milioni mbili) na wafanyabiashara wa vyakula vya mifugo.
Akizungumza na Sauti ya Istiqama Mshika fedha wa
ushirika huo Pili Nassor Kali amesema kuwa deni hilo limesababishwa kutokana na
kupanda kwa gharama za vyakula vya mifugo.
Mshika fedha huyo, amesema hapo awali gunia moja la
chakula cha mifugo hiyo, waliweza kulinunua
kwa bei ya shilingi elfu 25 ambapo kwa
sasa limepanda na kufikia shilingi elfu 47.
Aidha amesema, hukosekana kwa chakula hicho kwa
baadhi ya wakati kisiwani Pemba, hulazimika
kuwapatia chakula chengine ambacho hakina lishe bora kwa mifugo hiyo.
Amesema
kutokana na ukosefu wa fedha na kupanda bei kwa chakula hicho, walilazimika
kukopa katika maduka mbali mbali ambapo kwa sasa deni limeanza kuwazidi.
Kwa upande
wake Mjumbe wa ushirika huo Omar Abdallah Omar amesema hakuna faida yoyote
wanayoipat a kwa vile wameshindwa kugawana fedha walizozipata kutokana na mradi
huo kwa kuhofia hasara kubwa zaidi.
Hivyo
wameiomba serikali na taasisi binafsi kujitokeza ili kuweza kuwasaidia kuweza kujikwamua na deni hilo ,
ili ushiriika wao uweze kusonga mbele.
Ushirika huo
wa ufugaji wa kuku wa mayai, wenye lengo la kuwaendeleza mayatima waliopo
Mbuguani, umeanzishwa mwaka 2009, kwa
ufadhili wa Mfuko wa Maendeleo ya Jamii (TASAF) ukiwa na wanachama 11
MWISHO
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni