Habari

Ijumaa, 4 Oktoba 2013

Ripoti ya Benki ya Dunia yasema utalii unavutia uwekezaji na kuhimiza ongezeko la uchumi barani Afrika



Ripoti iliyotolewa na benki ya dunia inaonesha kuwa sekta ya utalii barani Afrika inavutia uwekezaji wa kikanda na wa kimataifa, na sekta ya utalii ni moja ya sekta zinazoleta faida kubwa duniani. 

Ripoti hiyo pia imesema sekta ya utalii barani Afrika inaweza kuchangia ongezeko zaidi la uchumi barani Afrika. Makamu mkuu wa benki barani Afrika Bw.

 Makhta Diop amesema mashirika binafsi yanavutia uwekezaji barani Afrika, na faida inayopatikana kutokana na kuwekeza barani Afrika ni kubwa. Ripoti hiyo imetolewa wiki moja wakati hoteli kubwa ya Ulaya Kempiski imetangaza kupanua uwekezaji wake katika bara la Afrika. 
Kwa sasa makampuni mengi ya kimataifa yanaongeza uwekezaji katika nchi za Afrika kusini mwa sahara, hasa nchini Kenya.

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni