Ndege ya kukodi imeanguka na kushika moto nje kidogo ya mji wa Lagos, nchini Nigeria, na kuuwa hadi watu 16. Maafisa wamesema watu sita wamenusurika na wamepelekwa hospitali, lakini wawili wako katika hali mbaya.
Msemaji wa idara ya safari za anga nchini Nigeria, amesema ndege hiyo ilikuwa imewachukua watu 20, abiria 13 na wafanyakazi saba.
Msemaji wa idara hiyo, Yakubu Dati, amesema kuwa ndege hiyo iliyotengenezwa nchini Brazil, chapa Embraer-120, ilianguka muda mfupi baada ya kuruka kutoka uwanja wa ndege wa Murtala Muhammed.
Ripoti za vyombo vya habari nchini humo zimesema kuwa ndege hiyo ilikuwa imewachukua waombolezaji na mwili wa marehemu, gavana wa zamani wa jimbo la Ondo Olusegun Agagu, ambaye alifariki Septemba 13.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni