Habari

Ijumaa, 4 Oktoba 2013

Sasa Nimemjua Nani Mkweli….!

Written by   //  03/10/2013  //  Habari  //  2 Comments

Baada ya kuuliza swali langu la juzi kuhusu nani mkwlei baina ya VP1 na VP2; nimeipata jawabu kutoka kwa Chikawe. Kumbe nilipiga indirect kick; then akina sahib zangu Makame Ame na wajumbe wengine wamechangia vizuri.
Ukweli hasa, ninaweza kusema kuwa ‘mkweli’ ilikuwa ninamjua hasa; ila……I was testing water.
Sasa, jamani ee- what next? Yaani huyu VP-000 anayeonekana dhahir kuwa ametupotosha na kutudanganya – afanywe nini? Ina maana ataendelea tu kukaa juu ya kiti huku akituadhibu roho zetu, anavunja sheria, anavunja katiba.
Math Chikawe, amesema ukweli; ila na yeye anazidi kujizonga maana aliwahi kukaririwa wiki moja kabla akisema kuwa anamtaka Rais Kikwete aitie saini rasimu/bill ile iliyochakachuliwa ‘halan abadan’.
Kwa hivyo, na yeye pia Chikawe anatakiwa awajibike au awajibishe, as a matter of principle — hii serikali (zote mbili) zinaonekana kuwa zimejaa uoza. urojo mtupu.
- Sasa, nini msimamo wa SMZ kw ajumla juu ya suala hili?
- Tujaalie Kikwete ataitia saini bill, itakuaje (kitu ambacho nafikiri anaweza, maana si mtu mwenye democratic values hizo) kuwa aone kitu wrong na akikatae, yeye ndiye huyo anayewatomeza CCM wenzake wafanye hayo wanayoyafanya.
- Je, BLW lina nguvu gani ya kukataa uoza kama huo, kama utaletwa baraza la wawakilishi (BLW). Yes/NO wanaweza kusema, neno? Au BLW litalaanishwa na kutiwa lubricants ilainike na hatimaye ipitishwe kwa mbwembwe.
- Je, msimamo wa CCM zanzibar wa akina Shaka Abdu Shaka, Sadifa, Vuai Ali Vuai, Shamsi Vuai Nahodha, Shawana Bukheit, Dr.Mohammed Gharib Bilali, akina Mama Asha Seif Ali Iddi, xalasinga (mzalendo); kada wa CCM (mzalendo) na wengine kama hao — utabaki kuwa wapi, “kama tulivyo” au vipi???
* Hivi kwa nini Mwenyekiti wa CCM taifa, haijawahi kutokea Zanzibar, wala hatokei huku mpaka kiyama.
* Hivi kwa nini Zanzibar hatupati Katibu Mkuu wa CCM taifa, hii haitokei wala haitokezi mpaka kiyama.
* Kwa nini Zanzibar tunaambulia kuwa na Naibu Katibu Mkuu, au Makamo Mwenyekiti wa CCM Zanzibar, na inakuwa attached na Makamo Mwenyekiti Bara, ambaye kimamlaka anaonekana kuwa ndiye BOSS. Kwa nini siku zote tunakuwa ‘surbodinates’ tu: hivi tuseme hatuwezi, hatuna akili au ndio ‘extension of imperial/empire/ukoloni wa Tanganyika’.

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni