Habari

Jumanne, 8 Oktoba 2013

Watu 40 wauliwa katika miripuko nchini Iraq

Jumanne, 08 Oktoba 2013 14:09
Watu 40 wauliwa katika miripuko nchini Iraq
Kwa akali watu 40 wameuawa nchini Iraq na makumi ya wengine kujeruhiwa baada ya kuibuka wimbi jipya la miripuko na ufyatuaji risasi. 

Vyombo vya usalama na duru za hospitali zinaripoti kwamba, miripuko kadhaa iliyotokea katika mji mkuu Baghdad imesababisha kwa uchache watu 40 kuuawa na wengine 80 kujeruhiwa. 

Polisi ya Iraq imetangaza kuwa, kwa uchache miripuko saba ya mabomu imetokea katika vitongoji vya Zaafaraniyah, Alam, Abidiyah, Daura na Saadiya mjini Baghdad. 

Miripuko hiyo imetokea siku moja tu baada ya Baghdad kushuhudia mauaji makubwa katika miripuko ya siku ya Jumamosi na Jumapili ambapo zaidi ya watu 100 waliuawa wakiwemo watoto wadogo. 

Licha ya kuwa hadi sasa hakuna kikundi chochote kilichotangaza kuhusika na mlolongo huo wa miripuko nchini Iraq, lakini kuna ishara ya kuhusika wanamgambo wanaofungamana na kundi la mtandao wa al-Qaeda.

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni