Habari

Ijumaa, 31 Januari 2014

ANC yakumbwa na tuhuma za kibaguzi A/Kusini

Frederik Willem  de Klerk  Rais wa zamani wa Afrika Kusini katika kipindi cha utawala wa ubaguzi wa rangi , amekituhumu chama cha African National Congress ANC nchini humo kwa kuanzisha  vitendo vya kibaguzi. 




Akizungumza mjini Cape Town hapo jana, de Klek ameongeza kuwa siasa hizo za ANC zinakinzana kikamilifu na katiba  ya nchi hiyo ambayo ina lengo la kuleta mshikamano wa kitaifa. 

Imeelezwa kwamba, kwa miongo kadhaa soko la ajira na uongozi wa mashirika ya nchi hiyo yalikuwa yakidhibitiwa na waupe wachache, hivi sasa chama cha ANC  kinaweka mikakati ya kuangaliwa upya suala la umiliki wa ardhi na mashamba yanayomilikiwa na weupe wachache nchini humo.

 Frederik de Klerk alikuwa rais wa saba na wa mwisho wa utawala wa makaburu nchini Afrika  Kusini amesema kuwa, wakati umefika wa kufanyika mazungumzo kati ya serikali na watu wote ambao wana azma ya kutekeleza mpango huo.

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni