Habari

Jumatatu, 20 Januari 2014

Mgombea Chadema ajisalimisha polisi.

Aliyetarajiwa kuwa mgombea wa udiwani wa Kata ya Mtae wilayaniLushoto kupitia Chadema na kutojitokeza kurejesha fomu hatimaye ajisalimisha polisi.


Mgombea huyo, Ali Said Jaha alijisalimisha juzi Jumamosi asubuhi katika Kituo cha Polisi cha Lushoto na kutoa maelezo kwamba hakuwa amepotea kama ilivyokuwa imeenezwa kwenye mitandao ya kijamii.
Alisema wakati wa kurejesha fomu siku ya Alhamisi Januari 16 mwaka huu kulikuwa na matatizo ya kifamilia nyumbani kwake  hivyo ikamlazimu kuyapa kipaumbele hatimaye akajikuta akiwa amechelewa kuwasili ofisi za Kata ya Mtae.

Sababu nyingine ya kutorejesha fomu kwa mujibu wa maelezo ya Ali alipokuwa akizungumza na gazeti hili kwa njia ya simu ni kuwa ilitokana na ndugu na jamaa zake wa karibu kumshauri kuachana na kugombea kwa sababu Chadema tayari kimepoteza mwelekeo kutokana na uongozi wa juukukwaruzana kila kukicha.
“Nilikuwa katika wakati mgumu sana, wazazi, ndugu na jamaa zangu wote walikaa kikao na kunishauri niachane na kugombea udiwani kupitia Chadema kwa sababu hatima yake haijulikani kutokana na kila kukicha
viongozi hawaishi kukwaruzana,” alisema Ali. Mgombea huyo alishindwa kutokea katika ofisi ya Ofisa Mtendaji wa Kataya Mtae kurejesha fomu kwa ajili ya kuingia katika kinyang’anyiro chakuwani nafasi hiyo hadi ulipofikia muda wa mwisho saa 10 jioni.
Kutotokea kwa mgombea huyo wa Chadema kulizua tafrani katika mitandaombalimbali ya kijamii.

Gazeti L Mwananchi

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni