Na Is-haka
Mohammed,Pemba. Licha
ya kuwepo kwa changamoto mbali mbali katika kuyaripoti matendo ya ubakaji
kumekuwepo na mabadiliko katika katika jamii jambo linalotia moyo ya kuwa iko
siku suala hili litatokomezwa katika hapa Zanzibar.
Akizungumza
na Zenj FM mratibu wa Chama cha waandishi wa habari wanawke
Tanzania(Tamwa-Zanzibar) Mzuri Issa amesema kumekuwepo na maendeleo kidogo kwa
jamii katika mtazamo wa kesi za ubakaji.
Amesema hiyo
ni kutokana na jamii kuanza kuwa na uelewa wa kuyaripoti matukio ya ubakaji
katika vyombo vya sheria baada ya elimu inayondelea kutolewa kwao kupitia
taasisi na wanaharakati mbali mbali ikiwemo TAMWA.
Aidha
Mratibu huyo amesema pia kumekuwepo na mabadiliko katika vyombo vya sheria ikiwemo
mahakama juu ya kuzichulia hatua kesi za ubakaji na baadhi ya kuanza kutolewa
hukumu ingawa amesema baadhi ya huhumu zimekuwa hadhirizishi kutokana na kesi
husika.
Hata hivyo
ameitaka jamii kuendelea kushirikiana na wanaharakati katika kuona suala hilo
ninatoweka kwa kuwafichua wale watu waovu wanaoendelea na matendao hayo katika
jamii,na kuwataka wasiwaonee muhali kwa vile si watu wema wanastahiki huruma
kwenye jamii.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni