KATIBU Mkuu Wizara ya Kilimo Zanzibar, Mhe: Afani Othman
Maalim akimpata maelzo Makamo wa Pili wa rais wa Zanzibar, Mhe:Balozi Seif Ali
Iddi, juu ya maendeleo ya shamba la Mikarafuu la Serikali lililoko makuwe
kisiwani Pemba.(Picha na Abdi Suleiman, PEMBA.)
Na Abdi Suleiman,PEMBA
MAKAMO waPili wa Rais wa Zanzibar, Mhe: Balozi Seif Ali Iddi, amitaka
Wizara ya kilimo na Maliasili Zanzibar, kuweka mikakati zaidi ya kusafisha
mashamba ya mikarafuu, kwa kuiyondoshea magugu yote iliyomo ndani ya mikarafuu,
ili mashamba hayo yaweza kuzaa vizuri.
Alisema kuwa, pindi magugu hayo yakiondoshwa basi mikarafuu
itawza kunawiri na kuza kwa wingi, kwani Zanzibar imekuwa ikitegemea zao hilo
kwa ajili ya mapato yake.
Balozi Seif aliyasema hayo huko, Makuwe wilaya ya Micheweni
mkoa wa kaskazini Pemba, mara baada ya kukagua shaba la Serikali la mikarafuu
katika ziara yake ya siku mbili kisiwani hapa.
Alisema kuwa, serikali inaamini kuwa bei ya zao hilo duniani
itaendelea kuwa nzuri, kwani tayari baadhi ya watu wameshaanza kuweka bunking
ya zao hilo.
Alisema kuwa, karafuu ya Zanzibar imekuwa ikipata hadhi kila
kukicha duniani kutokana na ubora wake, hivyo ni wajibu kwa wizara kuendelea
kuitunza mikarafuu, ili uchumu wa Zanzibar upate kuendelea.
“Tukiondosha karafuu Zanzibar yapili ni utalii, nao pia
unaingiza pato la nchi lakini karafuu ndio ya kwanza sasa kazi ya kuitunza na
kuisafisha ndio jambo la muhimu”alisema.
Aidha alifahamisha kuwa, Sera ya serikali iko pale pale juu
ya kuwapatia wananchi miche ya mikarafuu bure kama ilivyo fanya kwa msimu
uliopita ili kuwapa hamasa wananchi kupanda kwa wingi.
Balozi Seif alisema kuwa, suala la kukodishwa kwa mnada
shamba hilo, liendelee kwani ndio njia pekee nzuri, itayoepusha kutokea kwa
harufu ya rushwa wakati wa kukodisha kwa kutowa tenda.
“kukodishwa kwa mnada mtu anaona mwenyewe kitu kinachopigwa
bei, kuliko kutolewa tenda, kwani wananchi wengine kwa tenda hawapati
nafasi”aliongeza.
Hata hivyo aliitaka wizara ya kilimo, kuyatengea mafungu
mashamba hayo, wakati wa kusafishwa yasafishe vizuri ili karafuu zipate kuzaa
kwa haraka.
Kwa upande wake katibu mkuu wizara ya kilimo na mali asili
Zanzibar, Mhe:Afani Othman Maalim alisema kuwa samba hilo la makuwe lina
ukumbwa wa heka 200, tayari wameshapanda mikarafuu mipya 600 katika msimu huu.
Alisema kuwa lengo la kupanda mikarafuu hiyo, ni kuongeza
pato la nchi, ambapo kwa mwaka jana waliweza kuvuka kiwango kwa asilimia 104,
kuliko kiwango walichotakiwa kupata.
Alisema kuwa kwamsimu huu unaokwenda wanakadiria kupata
shilingi milioni 300 kuliko kiwango walichokiweka ZSTC, baada ya mavuno
kumalizika ya msimu unaofuata katika shamba hilo.
Aliyomba serikali, kuwapatia shilingi Milioni 35 kwa ajili
ya kulifanyia usafi shamba hilo, huku msimu uliopita wakipata faida ya shilingi
Milioni 110 baada ya kulikodisha shamba hilo.
MWISHO
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni