Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Kwanza wa Rais Fatma Abdulhabib Ferej akikabidhi visaidizi kwa watu wenye ulemavu kisiwani Pemba katika ghafla iliyofanyika katika uwanja wa Gombani.
Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Kwanza wa Rais Bi Fatma Abdulhabib Ferej akiwa katika pich ya pamoja na baadhi ya watu wenye ulemavu baada ya kukabidhi visaidizi mbali mbali nje ya uwanja wa Gombani Pemba.
Na Ussi Faki /PEMBA
Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamo wa Kwanza wa
Rais Fatma Abdulhabibi Fereji amewataka wasamaria wema, kuendelea kutowa misaada
ya hali na mali kwa watu wenye ulemavu kwani na wao ni sehemu ya jamii.
Hayo aliyaeleza
huko
uwanja wa Gombani Chake Chake Pemba alipokuwa akikabidhi vifaa mbali mbali kwa
baadhi ya watu wenye ulemavu wa aina
tofauti kutoka Wilaya nne za kisiwani Pemba.
Alisema
utowaji wa visaidizi hivo ni jukumu la kila mtu, kwani kufanya hivyo kunaweza kuwasaidi
watu hao hasa watoto hali ambayo itawarahisishia kupata elimu kwa urahisi
kutokana na visaidizi hivyo.
Aliwataka
wale ambao hawajapata visaidizi hivyo wasikate
tamaa kwani serekali inaendelea na juhudi ya kuwatafutia vifaa hivyo kwa njia
tofauti kwa vile bajeti ya serikali
haiwezi kuwapatia watu wote kwa wakati mmoja.
“Wale ambao hawakubahatika mwaka huu watapata
mwakani kwani hivi sasa tumesha wafahamu watu wenye ulemavu wote na pahali
walipo hivyo itakuwa rahisi kuwafikia na kuwapatia visaidizi” alisema Waziri Fatma.
Hata hivyo aliitaka jamii kuacha tabia ya
kuwaficha watoto wenye ulemavu kwani kufanya
hivyo ni kuwakosesha haki zao za msingi zikiwemo za kijamii,kielimu na nyenginezo
ambazo wana stahiki kuizipata katika
maisha yao yakila siku.
“Wazazi
ambao mmebahatika kupata watoto ambao wana ulemavu acheni tabia ya kuwaficha wenzetuhao
kwani kufanya hivyo ni kwenda kinyume na maadili ya dini”alisema waziri huyo.
Kwaupande
wake afisa mdhamini wa ofisi ya makamo wa kwanza wa Rais Pemba Fatma Muhamed
Omar alisema utowaji wa visaidizi hivyo ulizingatia ushauri wa dakitar kwa
kutaka kujuwa yupi anafaa kupewa kulingana na hali ya ulemavu alio nao.
Akitowa
salamu za shukrani kwa kupata visaidizi hivyo kwa niaba ya watu wenye ulemavu
wenzake Atie Sulemani Salum ameishukuru serekali ya Mapinduzi ya Zanzibar kwa
kuwapa visaidizi hivyo na kuiomba kuendeleza kuwasaidia zaidi kwani misaada kwa
watu hao ni kitendo cha kuendelea.
Katika hafla
hiyo Waziri alikabidhi vifaa kama vile
magongo ya kutembelea peya 72,Fimbo nyeupe 36,Viti vya magurudumu mawili
16,Miwani pamoja na kofia kwa watu wenye ulemavu wa ngozi 36.
MWISHO.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni