Habari

Jumapili, 19 Oktoba 2014

WAKULIMA WA TUNGULE(NYANYA) MWAMBE WALIA NA WADUDU WAHARIBIFU,WAIOMBA SERIKALI KUWAPELEKEA WATAALAMU,



 Shamba la mitungule lililopo Mjikunju katika Shehia ya Mwambe Mkoani.
Baadhi ya mitungule iliyoathiriwa na wadudu huko katika shamba la wakulima Mwambe.



Na Ussi Faki PEMBA                                                                                                                                 Wakulima wa tungule wa shehiya  ya  Mwambe Wilaya ya  Mkoani  Pemba wameiomba Serekali kuwapatia wataalamu wa kilimo cha tungule ili kuwasaidia  kuondosha tatizo la wadudu wa aina ya  Dumunzi linalo kikabili kilimo hicho .
Hayo waliyaeleza badhi ya wakulima wa zao hilo huko kijijini  Mjikunju Mwambe  walipokuwa wakizungumza na mwandishi wa Habar hizi alipofika kijijini huko.
Mkulima  Iliasi Koti alisema kuwa wao hutumia nguvu nyingi hasa wakati wanapo taarisha mashamba kwani huwabidi kutumia nguvu pamoja na pesa kwa kulimisha ili wapatemavuno mazuri.
Alisema zao la tungule ni zao ambalo wanalipenda  kwani ndilo linalo wapatia kipato  lakini kwa  sasa limekuwa gumu kutokana na kuingiwa na wadudu hao wa Dumuzi  na kuvamia mazao yao kwa kasi kubwa.
Hatahivyo alisama halihiyo imemkatisha tamaa msimu huu   kwa kuliacha shamba lake liliopo makaani kutokana na kushambuliwa na wadudu hao wa aina ya Dumuzi.
“nimeliacha shamba mimi kutokana na wadudu hawa ambao wanapo ingia shambani huwezi kupata kitu chochote kutokana na wimbi la ugonjwa wanao ingiza katika mitungule” alisema koti.
Naye Khamis BakarKhamis alisema kilimo cha Tungule kwasasa kinawapa tabu kutoka na ukosefu wa  elimu ya kilimo hicho, hivyo huwabidi kutumia madawa kwa kubahatisha.
Alisema elimu huhitajika kuazia pale wanapo weka mbegu katika kitalu na kuitowa mche kuipeleka katika shamba hali ambayo huwasumbuwa na kuwafanya kununuwa madawa katika maduka ya dawa za kilimo  kwa kubahatisha kua baadhi ya wakati hubahatika na wakati mwengine hufa.
Kwa upande wake mkulima Omar Sadi alisema wanajitahidi kulima lakini tatizo kubwa kuhusiana nawadudu  dumuzi na huwafanya kutumia fedha nyingi kununuwa madawa jambo ambalo huwapa hasara kumbwa kutokana na kutofikiwa na mabwana shamba.
Hatahivyo wakulima hao walieleza changa moto zinazo wakabili ikiwemo ukosefu wa  mbegu bora , madawa, mbolea ,elimu jambo ambalo linawakosesha kukihimili kilimo hicho ambacho huwapatia kipato cha kujikimu kimaisha pamoja na familia zao.
                                                        MWISHO   

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni