Baadhi ya waandishi wa habari wakimsikiliza Kaimu Kamanda wa
Polisi Mkoa wa Kusini Pemba Ali Hamad Said wakati alipokuwa akitoa taarifa ya
kuokotwa kwa maiti huko katika kijiji Matale Pemba katika Makao ya jeshi la
Polisi Mkoa wa Kusini Pemba.
Na Is-haka Mohammed,Pemba.
Mtu
mmoja mwanamme mwenye umri wa miaka 42 mkaazi wa Kinowe Konde amekutwa
amefariki dunia katika msitu uliopo baina ya eneo la Matale na chambani mkoa wa
kusini Pemba.
Kaimu kamanda wa polisi mkoa wa kusini Pemba ambaye ni Mkuu
wa Upelelezi Mkoa huo Ali Hamad Said amesema
maiti hiyo ambayo ilikuwa imeshaharibika iliokotwa juzi tarehe 28/10/2014 majira ya saa kumi na nusu za jioni katikati yam
situ huo.
Alimtaja marehemu kuwa ni Mjaka Mmanga Mjaka anayesadikiwa
kuwa ni mgojwa wa akili ambapo inaelezwa kuwa alikuwa akielekea Chambani ambako
kuna wake zake na alikuwa na kawaida ya kwenda mara kwa mara.
Kaimu Kamanda huyo amesema mwili wa marehemu ulilazimika
kuzikwa katika eneo hilo hilo kutokana na kuwa mwili wake ulishaharibika sana
na kutowezekana kuuhamishia katika eneo jengine kwa mazishi.
Amesema awali mwili huo ulikuwa haujatambulika kutokana
kuharibika kwake,lakini kutokana na kusambaa kwa taarifa uliweza kutambulika.
Wakati huo huo Jeshi la Polisi mkoa wa kusini Pemba linamshikilia
mtu mmoja ambae jina lake linahifadhiwa kwa shughuli za kiupeleleziakisadikiwa kumshambulia Suleiman humud Suleiman mkazi wa
Chanjamjawiri Wilaya ya Chake Chake kwa Mapanga nakusababishiamaumivu makali.
Kaimu Kamanda huyo amesema tukio hilo lilitokea tarehe 21
mwezi huu ambapo lilisababisha Suleiman kulazimika kuhamishiwa katika Hospitali
ya Taifa ya Muhimbili baada ya kushindikana kutibiwa katika hospitali za Chake
Chake na Mkoani Pemba.
Hata hivyo ameeleza baada ya kufikishwa katika hospitali ya
Muhimbili na kupatiwa matibabu hali yake iliimarika na kuweza kuwataja watu
waliomshambulia na hatimaye mmoja kati ya hao ndiye anayeshikiliwa huku jeshi
la polisi likiwasaka wengine kwa ajili ya kuwafikisha katika vyombo vya sheria.
Kwa upande mwengine Kamanda Said amewataka wananchi
kutochukua sheria mikononi mwao kutokana na tukio hilo kuonekana na kulipiza
kisasi kutokana na kutochukuliwa kwa mali yeyote licha ya kuwa na Baskeli,simu
na pesa mfukoni mwake.
Amesisitiza kuwa jeshi la polisi linaendelea kufanya
upelelezi ili kuwafichua wahalifu katika matukio mbali mbali ya kihalifu yanayoendelea
kujitokeza katika maeneo tofauti ya kisiwani Pemba ikiwemo kijiji
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni