Habari

Alhamisi, 23 Oktoba 2014

WANAFUNZI ZAIDI YA 200 NA WALIMU WAO WANAJISAIDIA KWENYE CHOO KIMOJA SINGIDA


Wanafunzi zaidi ya mia mbili hamsini na walimu zaidi ya kumi na tano wa shule ya sekondari Mandewa iliyopo katika manispaa ya Singida haina vyoo,jambo ambalo linawalazimu kuchangia katika choo cha kantini tokea shule hiyo  ilipoanzishwa mwaka elfu mbili na sita. 
Wakieleza walimu na wanafunzi katika harambee iliyo itishwa na shule hiyo kuchangia matatizo mbalimbali ikiwemo ujenzi wa maabara wamesema ni jambo la aibu mwanafunzi kukutana na mwalimu katika choo kimoja.
 
Akielezea changamoto katika shule yake mkuu wa shule ya sekondari Mandewa Bi. Magreth Misanga amesema ukosefu wa vyoo vya walimu katika shule yake imekuwakero kwa walimu kwani ina walazimu kutumia choo kimoja na wanafunzi.
 
Kwa upande wake mgeni rasmi katika harambee hiyo rais wa shirikisho la  wachibaji madini Tanzania Bwana John Bina, pamoja na  kuwata walimu wasivunjike moyo kufundisha amewachangia malori saba ya mchanga na shilingi laki tano kwa ajili ya ujenzi wa vyoo ,ili kuondoa tatizo la hilo la kuchangia choo wanafunzi na walimu.
 
Katika harambee hiyo zaidi ya shilingi laki saba mifuko ya saruji  ishirini na tano pamoja na lori saba za michanga vimepatikana.

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni