Habari

Alhamisi, 16 Oktoba 2014

Wizara ya afya Zanzibar imejiandaa vyema kuwapatia chanjo watoto


Wizara ya afya Zanzibar imejiandaa vyema kuwapatia chanjo za Minyoo, Surua na Rubela na Vitamen ‘A’ kwa watoto wenye umri wa miezi sita hadi umri wa chini ya Miaka 15 kuanzia Oktoba 18 hadi 24 mwaka huu.

Akizungumza na zenji fm radio huko ofisini kwakwe Chake Chake, Afisa Ufuatiliaji Magonjwa yanayokingwa kwa chanjo Kisiwani Pemba, Bakar Hamad Bakari amesema maandalizi yote ya utoaji wa Chanjo yameshakamilika kiswani humo.
Aidha amefahamisha kuwa, lengo la wizara ya afya kuchanja watoto kwa zaidi ya asilimia 95 wenye umri kati ya miezi sita mpaka chini ya umri wa miaka 15.
Bakari amewataka viongozi mbali mbali kisiwani pemba kuhamasisha jamii kujitokeza katika kuwapatia chanjo watoto wao ili wakuwe katika afya bora na kuwakinga na maradhi mbali mbali.

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni