Habari

Ijumaa, 7 Novemba 2014

Kaiza:wasomi ikataeni katiba mpya


Wasomi nchini wametakiwa kuikataa rasimu pendekezi ya katiba mpya kwa kuipigia kura ya hapana mara utakapofika wakati wa wananchi kutoa maamuzi juu ya katiba hio.

Kauli hio imetolewa na Makamo mwenyekiti wa Jumui ya vijana CUF Taifa(JUVICUF) Mh.Yussuf Kaiza Makame wakati akizungumza na wasomi wa vyuo mbali mbali Zanzibar katika ukumbi wa Salama Hall Bwawani.
Mh.Kaiza aliwatanabahisha wanafuzi wa vyuo vikuu kuacha woga kwani siasa ni haki yao ya msingi hivyo kuendelea na woga ni sawa na kupoteza haki yao ya kikatiba na kibinadamu.

Pamoja na hayo aliwahakikisha wasomi hao kuwa ifikapo mwaka 2015 hakuna wakumzuia Maalim Seif asingie ikulu kwani dalili zipo wazi kwa sasa kutokana na kiongozi huyo kuendelea kukubalika zaidi juu ya sera zake za kudai haki ya kila mzanzibar.
Aidha alitoa salamu kwa Chama cha Mapinduzi CCM kujifunza kupitia Bukinafaso ambapo wananchi kwa sasa wameamua kuchukua serikali yao wenyewe kupitia maandamano ya siku moja nzima hivo jambo kama hilo linaweza kutokea pia kwa Zanzibar iwapo haki haitotendeka.
Akitoa nasaha zake kwa wasomi hao mgeni rasmi katika hafla hio Katibu mkuu wa Chama cha Wananchi CUF ambae pia ni Makamo wa kwanza wa Rais Zanzibar,Maalim Seif Sharif Hamad aliwataka wasomi hao kukataa kabisa kubaguliwa kwani sera za ubaguzi zimepitwa na wakati kwa sasa.
Pamoja na hayo alisema katiba iliopitishwa na Bunge la Katiba haina maslahi kwa wazanzibar hivo ni wajibu kwa wasomi hao kuikataa katiba hio ifikapo wakakati wa kuipigia kura.
Akisoma risala ya kwa niaba ya wanafunzi hao mmoja wa wananfunzi wa Chuo kikuu cha Zanzibar University Hafidh Ali Hafidh alisema wao kama wasomi hawawezi kuikubali rasimu hio kwani haina usawa kwa pande mbili za Muungano.
‘’Tunaikataa katiba pendekezi kwa sababu haina maslahi na Nchi yetu na katu sisi kama wasomi hatuwezi kuikubali’’alieleza msomi huyo.
Nae mratibu wa shughuli hio ambae pia ni msomi wa mwaka wa tatu katika chuo kikuu cha Zanzibar University Bi Moza Nassor Hemed alimuhakikishia Maalim Seif kuwa wanafunzi wapo macho na harakati mbali mbali za kuidai Zanzibar kupitia katiba mpya na wanaiunga mkono CUF kwa kila jambo.
Alisema wao kama wasomi watahakikisha wanaipigia kura ya hapana katiba hio kwa sabau haina usawa wowote hule wa pande mbili za Muungano na lolote lile litakalokuwa basi wapo tayari kukabiliana nalo.
Mdahalo huo uliofanyika katika ukumbi wa salama hall bwawani mnamo tarehe 2/11/2014 uliwashirikisa wanafunzi wa vyuo zaidi ya 2000 Zanzibar ambapo pia Maalim Seif alipata nafasi ya kuwakabidhi kadi za chama wanachama wapya 380 miongoni mwa wasomi hao.

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni