Habari

Jumatano, 5 Novemba 2014

WANANCHI KISIWANI PEMBA WASEMA SUK BADO INA CHANGAMOTO.


Na Is-haka Mohamed,Pemba.                                                                                                                                                                                Baadi ya wananchi kisiwani Pemba wamesema serikali ya Zanzibar iliyo chini ya mwemvuli ya Umoja Kitaifa bado inakabiliwa na changamoto nyingi ikiwa ni pamoja na kuwepo kwa maelewano mazuri kwa viongozi wanaunda serikali hiyo iliyo chini ya CCM na CUF.

Wakizungumza na Blog hii baadhi ya wananchi hao wamesema kuwepo kwa maneno ya kushutumiana katika majukwaa ya kisiasa kunadhihirisha kuwepo kwa mpasuko kati ya pande hizo mbili.
Walisema licha ya Rais Dk Ali Mohamed Shein kutimiza miaka minne ya uongozi wake bado kunawaweka njia panda wananchi juu ya serikali hiyo ambayo walidai walikuwa na matumaini makubwa na serikali ya umojawa kitaifa wameanza kupata hofu ya kutokana na kauli za viongozi hao.
Ali Said Moh`d wa Chake  Chake alisema licha ya kuendelea kuwepo kwa amani na utulivu bado katika hali ya maisha ya wananchi yapo chini na tatizo la ajira ,umaskini wa kipato kwa wananchi,kushutumiana wazi wazi kwa viongozi kunazidisha hofu kwa wananchi waliowengi.
“Kweli serikali ya umoja wa kitaifa imeleta mshikamano kwa wananchi na kuondosha tofauti zetu,kwani sasa tunazikana,tunashirikiana katika shughuli za kijamii,lakini tunasema uwajibikaji wa viongozi kwa wananchi haupo”alisemaMoh`d.
Katika hatua nyengine mwananchi huyo amekerwa na malumbano ya viongozi wa Zanzibar juu ya katiba inayopendekezwa  na kuwaomba viongozi hao kushikiana na kuwaunganisha wananchi wote juu ya kupata katiba itakayokuwa na maslahi ya Zanzibar na sio kuvutiana katika maslahiya vyama vyao.
Mwalim Said Hamad Malik wa Kiuyu Wilaya ya Wete amesema kuwa matumaini waliyoyategemea kutokana na serikali ya umoja wa kitaifa yametoweka kwa vile viongozi wanajivutia wao wenyewe na kuwasahau wananchi ambao ndio waliwaweka madarakani.
Aidha alisema  masheha bado wanafanya kazi ya kuwabagua wananchi kwa misingi ya vyama vyao kwa kuwakosesha fursa muhimu kama nafasi za ajira,kushiriki katika miradi inayokwenda katika shehia zao na kuweza kuwapatia vijana wenye itikadi zao.
“Sisi huku ilikuwa hatuzikani kutokana na itkadi za vyama sasa kuja kwa serikali hii ya umoja wa kitaifa lakini masheha wetu wanaendelea na vitendo hivyo vya kuwabagua wananchi”Alifahamisha Malik.
Aidha amesema viongozi wa majimbo wawakilishi na wabunge wanashindwa kutimiza majukumu yao na hatimaye kutoonekana kabisa katika majimbo yao na kuwaacha wananchi wakiwa nyuma kimaendeleo kwa kushindwa kutekeleza ahadi kemkem walizozitoa wakati wa kampeni.
Amesema huduma nyingi za kijamii katika majimbo kama vile miundombinu ya barabara,afya,maji safi n sala,skuli  imedumaa kutokana kutokuwepo wa kuyasimamia na kuyaendeleza.
Akifungua Kongamano  liloandaliwa na Chama Cha Mapinduzi (CCM) katika maadhimisho ya miaka minne tangu alipoingia madarakani Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein alisema anajivunia mafanikio katika uongozi wake, na jambo kubwa zaidi ni kuimarika kwa hali ya amani na utulivu wa nchi.

Alisema atahakikisha Zanzibar inabaki salama na suala la amani na maendeleo halina mbadala, hivyo atahakikisha amani inadumu kwani bila ya amani hata ibada hazitafanyika.

Alisema wengi walidhani atakwazwa na hataweza kuiongoza Zanzibar, lakini ameweza na kwa mafanikio makubwa na kuleta maendeleo, hivyo anajivunia hilo.

“Wapo walotubeza kusema kuwa mipango yetu haitekelezeki ya ilani ya Chama Cha Mapinduzi na wapo walopiga kelele kuwa nimeunda serikali kubwa kwa sababu ya wingi wa wizara, niwaambie kuwa wingi wa wizara siyo serikali, ” alisema Dk. Shein.  

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni