Na Is-ha
Mohammed,Pemba. Naibu Mwenyekiti wa Mahakama ya Ardhi Pemba Salum Hassan Bakari amesema
ni wajibu wa kila mmoja kuhakikisha amani ya nchi iliyopo inatuzwa ili
kuendelea kuwepo na amani na utulivu nchini.
Mh. Hassan
ameyasema hayo leo huko Madungu Chake Chake wakati akifungua Kongamano juu
ya maadhimisho ya siku ya Amani duniani
lililoandaliwa na Jumuiya ya Vijana ya Umoja wa Mataifa(YUNA Pemba) kwa
kushirikiana na Jumuiya ya Waandishi wa Habari wa kujitegemea Pemba (PFO).
Amesema
jukumu la kulinda Amani ya Nchi ni Serikali,lakini jukumu zaidi linaangukia kwa
wanajamii wenyewe kwa vile watu wanaoshiriki katika matendo ya uvunjifu wa
amani wanatoka ndani jamii iliyowazunguka.
Amesema
matendo yanayoendelea kuibuka Zanzibar na Tanzania kwa jumla ya kumwagiwa watu
tindikali, licha ya kuwa ya kikatili bali yanaweza kuipeleka nchi katika
uvunjiwa wa amani na utulivu uliomudu kwa muda mrefu.
Amesema ni
busara kwa Watanzania kuondoa tafauti
zao za kisiasa,kidini,kikabina na kikanda na kuungana kuwafichuwa watu
wanaendelea kuhatarisha amani na utulivu uliopo nchini.
Akichagia
katika Kongamano hilo Mwenyekiti wa Jumuiya ya Madereva Mkoa wa Kusini Pemba
Mw. Moh`d Ali Shela amesema ili elimu
isaidia katika kuleta maendeleo ya amani nchini serikali inatakiwa kuchukuwa
juhudi za makusudi kupambana na suala la ukosefu wa ajira nchini, sambamba na
kupunguza mfumuko wa bei za bidhaa hasa za chakula.
Amesema kuwa
kuwepo kwa ukosefu wa ajira kwa jamii kunapelekea vijana kujiingira katika
vitendo vya utumiaji wa madawa ya kulevya,wizi na vitendo vyengine viovu
hatimae kusababisha kutoweka kwa amani nchini.
Aidha ameisa
jamii kutojiingiza katika vitendo vya uvunjifu wa amani kwa vile amani
ikivunjika hakuna chochote kitakachoweza kufanikiwa,kwa vile shughuli zote za
kimaendeleo kama vile kilimo,biashara na
nyenginezo hazitoweza kufanyika na kusababisha njaa na ukame katika nchi huku
akitolewa mfano katika nchi za Syria na Somalia.
Naye Mrati
wa YUNA Pemba Mw. Mohammed Hassan ameitaka serikali kuweka mikakati madhubuti
ya kukabiliana na uvunjifu wa amani nchini,huku akitowa wito kwa walimu mashuleni
kutoa elimu ya umuhimu wa amani kwa wanafunzi.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni