Habari

Jumamosi, 21 Septemba 2013

Waandishi wapata Semina ya Kuripoti Sheria za Utambuzi wa Ardhi Zanzibar.




 Mratibu wa Mafunzo ya kuripoti Utambuzi wa Sheria za Ardhi Zanzibar Ali Rashid, akitpowa  mada kuhusu matumizi ya Ardhi na jinsi ya kufanyiwa Utambuzi kwa mmiliki halali wa ardhi, mafunzo hayo yaliwashirikisha waandishi wa habari mbalimbali Zanzibar, wakati kukiwa na zoezi la Utambuzi wa Ardhi na Usajili linalofanyika katika Wilaya  za Unguja.
 Mtoa Mada AliRashid akisisitiza jambo wakati wa mafunzo hayo kwa  waandishi wa habari yaliofanyika katika ukumbi wa Idara ya Habari Kikwajuni Zanzibar.
 Afisa Mtambuzi wa Ardhi Zanzibar Shawana Soud Khamis, akitowa mada ya kisheria jinsi ya Utambuzi wa Usajili wa Ardhi unavyofanyika na kumpata mmiliki halali, zoezi hilo linafanyika katika maeneo mbalimbali ya Zanzibar, likiazia katika Wilaya za Kati na Mjini kusajili Ardhi na kupata Wamiliki wa ardhi halali na kupata hati miliki ya Ardhi anayomiliki na kutambuliwa Kisheria.
 Waandishi wakifuatilia mafunzo hayo ya kuripoti habari za Usajili wa Ardhi Zanzibar, linalofanyika katika wilaya mbalimbali za Unguja.

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni