Habari

Ijumaa, 4 Oktoba 2013

Jimbo jingine Ujerumani lautambua rasmi Uislamu

Ijumaa, 04 Oktoba 2013 09:10

Jimbo jingine Ujerumani lautambua rasmi UislamuJimbo la Niedersachsen moja kati ya majimbo 16 nchini Ujerumani, limeitambua dini ya Kiislamu kuwa ni dini rasmi kwenye jimbo hilo lililoko kaskazini magharibi mwa nchi hiyo. Taarifa zinasema kuwa, jimbo la Niedersachsen linakuwa jimbo la tatu baada ya Bremen na Hamburg kuitambua rasmi dini ya Kiislamu nchini humo. Stephen Weil, kiongozi mwandamizi wa serikali ya jimbo hilo amesema kuwa, Waislamu katika jimbo hilo, ni sehemu muhimu ya wananchi, na kusisitiza kwamba serikali ya jimbo ina azma thabiti ya kuwaheshimu Waislamu na matukufu yao. Wakati huohuo, Mkuu wa Baraza la Mji wa Hanoever amesema kuwa,  Waislamu ambao wanaunda asilimia saba ya wananchi wa jimbo hilo wana haki ya kupata haki zao kisheria kama ilivyokuwa kwa wafuasi wa dini za Kikristo na Kiyahudi katika eneo hilo.

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni